From Wikipedia, the free encyclopedia
Lorenzo de' Medici (tamka me-di-chi; 1 Januari 1449 - 8 Aprili 1492) alikuwa mfanyabiashara na mwanasiasa katika mji wa Firenze (kwa Kiingereza: Florence) nchini Italia wakati wa karne ya 15. Aliitwa pia na watu wa mji wake Lorenzo il Magnifico (Lorenzo adhimu)[1]. Lorenzo alizaliwa katika familia ya Medici waliokuwa wafanyabiashara tajiri na babu yake Cosimo de' Medici aliwahi kupanda ngazi kuwa mtawala wa Firenze.
Firenze ilikuwa wakati ule dola-mji na jamhuri ya kujitegema iliyokuwa tajiri kutokana na biashara yake ya kimataifa; ilikuwa kitovu cha kiuchumi ambako benki za kwanza za Ulaya zilipoundwa. Utajiri wa mji uliwezesha taasisi za elimu na kazi ya wasanii wengi, na familia ya Medici ilikuwa kati ya wafadhili mashuhuri zaidi wa elimu na sanaa wakati wa Zama za Mwamko.
Lorenzo alitumia utajiri wake kuwa kiongozi halisi wa siasa ya Firenze ingawa hakuchaguliwa katika ofisi yoyote[2]. Wakati wake viongozi waliochaguliwa katika halmashauri ya serikali ya jamhuri hiyo walimtegemea kifedha na kisiasa. Anajulikana zaidi kwa ufadhili wake wa wasanii mashuhuri kama vile Sandro Botticelli na Michelangelo Buonarroti. Ufadhili huo na ujenzi wa majengo mazuri kama makanisa na majumba ulikuwa sababu ya kumwita "il magnifico" (mwadhimu).
Lorenzo mwenyewe alikuwa pia msanii aliyetunga mashairi. Alizaa watoto 10 na mmojawao aliyeitwa Giovanni akawa Papa Leo X.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.