From Wikipedia, the free encyclopedia
Kuua kwa kukusudia (kwa Kiingereza: murder) ni kosa la jinai kadiri ya sheria ambapo mtu mmoja anasababisha kifo cha mtu mwingine kwa makusudi na kwa nia mbaya.
Sheria ya Tanzania inafafanulia: "Mtu yeyote ambaye, kwa dhamira ya uovu, anasababisha kifo cha mtu mwingine kwa kitendo kisicho halali au kuacha kutenda ana hatia ya kuua kwa kukusudia."[1]
Adhabu ya kuua kwa kukusudia ni adhabu ya kifo[2], ingawa adhabu hiyo haijatekelezwa tena Tanzania tangu mwaka 1994[3], nchini Kenya tangu 1987, Uganda tangu 2005 https://www.pgaction.org/ilhr/adp/uga.html[4].
Idadi ya nchi zilizofuta adhabu ya kifo inazidi kuongezeka[5].
Katika sheria za kisasa uuaji wa makusudi hutazamwa kama jinai dhidi ya jamii unaopaswa kuadhibiwa na dola. Katika mifumo ya sheria ya kimapokeo ulitazamwa mara nyingi kama jambo la binafsi, pia kwa kutotofautisha kati ya kuua kwa kusudi na bila kusudi; hapo ukoo wa aliyeuawa alikuwa na haki ya kulipiza kisasi kwa kumwua muuaji au ndugu wake. Ili kupakana marudio ya kisasi mifumo mingi ya kimapokeo ilijua pia malipo ya fidia.
Mfumo wa fidia unapatikana katika nchi kadhaa (mfano Iran, Saudia, Pakistan) zinazofuata sharia ya Kiislamu ambako ni juu ya familia ya aliyeuawa kuamua kuhusu fidia au utekelezaji wa adhabu ya kifo.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.