Vitaumande ni ndege mbuai wa jenasi mbalimbali wa nusufamilia Surniinae katika familia Strigidae. Ndege hawa ni wadogo kuliko bundi (sm 12-28) na wana rangi ya kahawa au kijivu pamoja na miraba au madoa.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...
Kitaumande |
Kitaumande miraba |
Uainishaji wa kisayansi |
Himaya: |
Animalia (Wanyama)
|
Faila: |
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
|
Ngeli: |
Aves (Ndege)
|
Oda: |
Strigiformes (Ndege kama bundi)
|
Familia: |
Strigidae (Ndege walio na mnasaba na bundi)
|
Nusufamilia: |
Surniinae (Ndege walio na mnasaba na bundi-panga)
|
Jenasi: |
Aegolius Kaup, 1829
Athene Boie, 1822
Glaucidium Boie, 1826
Micrathene Coues, 1866
Xenoglaux O'Neill & G.R. Graves, 1977
|
Spishi: |
Angalia matini
|
|
Funga
Vitaumande hula panya na wanyama na ndege wadogo wengine na hata watambaazi wadogo, popo, samaki, wadudu na nyungunyungu. Kulingana na spishi huwinda wakati wa alasiri au alfajiri au hata mchana na pengine usiku.
Jike huyataga mayai 2-7 katika tundu lililoachwa na ndege au mnyama mwingine, mara nyingi lile la kigong'ota au zuakulu. Spishi fulani huchimba vishimo katika ardhi au nyingine hutaga ndani ya matundu katika miamba, kingo za mito au majengo makuukuu au hata ndani ya vishimo vya sungura.
- Athene noctua, Kitaumande wa Athena (Little owl)
- Athene superciliaris, Kitaumande wa Madagasska (White-browed owl)
- Glaucidium albertinum, Kitaumande-mlima (Albertine owlet)
- Glaucidium capense, Kitaumande Miraba (African barred owlet)
- Glaucidium c. ngamiense, Kitaumande wa Ngami (Ngami owlet)
- Glaucidium c. scheffleri, Kitaumande wa Scheffler (Scheffler's owlet)
- Glaucidium castaneum, Kitaumande Kahawiachekundu (Chestnut owlet)
- Glaucidium etchecopari, Kitaumande wa Kodivaa (Etchecopar's owlet)
- Glaucidium perlatum, Kitaumande Madoa (Pearl-spotted owlet)
- Glaucidium sjostedti, Kitaumande Mkia-miraba Sjöstedt's barred owlet)
- Glaucidium tephronotum, Kitaumande Kidari-chekundu (Red-chested owlet)
- Athene megalopeza (Mwisho wa Pliocene ya Rexroad, MMA) – pengine inawekwa katika Speotyto
- Athene veta (Mwanzo wa Pleistocene ya Rebielice, Poland)
- Athene angelis (Kati mpaka mwisho wa Pleistocene ya Castiglione, Korsika)
- Athene trinacriae (Pleistocene)
- Athene cf. cunicularia (Pleistocene ya Barbuda, Bahari ya Karibi) – pengine inawekwa katika Speotyto
- Athene cf. cunicularia (Pleistocene ya Visiwa vya Cayman, Bahari ya Karibi) – pengine inawekwa katika Speotyto
- Athene cf. cunicularia (Pleistocene ya Jamaica, Bahari ya Karibi) – pengine inawekwa katika Speotyto
- Athene cf. cunicularia (Pleistocene ya Kisiwa cha Mona, Bahari ya Karibi) – pengine inawekwa katika Speotyto
- Athene cf. cunicularia (Pleistocene of Puerto Rico, Bahari ya Karibi) – pengine inawekwa katika Speotyto
- Athene cretensis (Cretan Owl, mwisho wa Quaternary ya Kreta, Bahari ya Mediteranea)
Kitaumande wa Athena
Kitaumande madoa
Northern Saw-whet Owl
Boreal Owl
Buff-fronted owl
Spotted Owlet
Burrowing owl
Ferruginous pygmy owl
Collared owlet
Northern pygmy owl
Costa Rican pygmy owl
Asian barred owlet
Mountain pygmy owl
Amazonian pygmy owl
Andean pygmy owl
Austral pygmy owl
Cloud-forest pygmy owl
Colima pygmy owl
Eurasian pygmy owl
Pacific pygmy owl
Jungle owlet
Cuban pygmy owl
Forest owlet
Elf owl