Mwandishi wa Denmark From Wikipedia, the free encyclopedia
Karen Christence Blixen-Finecke (jina la kiuandishi alilotumia kwenye nchi zinazozungumza Kiingereza: Isak Dinesen) (Rungsted/ Denmark 17 Aprili 1885 - 7 Septemba 1962) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Denmark. Alitumia pia majina ya Tania Blixen, kwenye nchi zinazozungumza Kijerumani, Osceola na Pierre Andrézel.
Aliishi Kenya -wakati ule: Afrika ya Mashariki ya Kiingereza- kati ya 1913 hadi 1931 akiongoza shamba la kahawa karibu na mji wa Nairobi. Eneo la shamba lake la zamani hadi leo laitwa "Karen" ni kitongoji cha Nairobi.
Aliandika kumbukumbu ya maisha yake Kenya na kitabu hiki kikawa msingi wa filamu "Out of Africa". Huko Denmark alijulikana sana kwa kazi yake iitwayo Seven Gothic Tales.
Karen Dinesen alizaliwa Rungstedlund, kaskazini mwa Copenhagen. Baba yake, Wilhelm Dinesen (1845–1895), alikuwa ni mwandishi na ofisa wa kijeshi toka familia ya wamiliki wa mashamba ya Jutland yenye uhusiano wa karibu na ufalme, kanisa na siasa za mrengo wa kulia. Mama yake, Ingeborg Westenholz (1856–1939), alitoka kwenye familia tajiri inayofanya biashara. Karen Dinesen alikuwa ni mtoto wa pili kati ya watoto watatu wa kike na wawili wa kiume. Mdodo wake wa kiume, Thomas Dinesen, alipata tuzo ya Victoria Cross wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.[1] Dinesen was known to her friends as "Tanne".
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.