From Wikipedia, the free encyclopedia
Kanuni ya Imani ya Mitume (kwa Kilatini: Symbolum Apostolorum au Symbolum Apostolicum) ni ungamo la imani ya Ukristo lililoanza kutumika mjini Roma katika karne ya 2 kwa ajili ya ubatizo, halafu likaenea hasa katika Kanisa la Magharibi.[1]
Kanuni hiyo inaendelea kutumiwa na Kanisa Katoliki na madhehebu mengi ya Uprotestanti katika liturujia na katekesi.
Kwa kuwa ilitokea Ulaya Magharibi, ambapo elekeo la kinadharia si kubwa kama huko Ugiriki, tena mapema kuliko mabishano mengi ya teolojia kuhusu umungu wa Yesu Kristo na wa Roho Mtakatifu, haina ufafanuzi wa kina.
Maandishi ya zamani zaidi tuliyonayo yanayoitaja "Kanuni ya Imani ya Mitume" ni barua ya mwaka 390 hivi kutoka sinodi ya Milano kwa Papa Siricius.[2][3][4]
Imani ya Mitume (umbo la Kanisa Katoliki)[6] | Imani ya Mitume (umbo la Kanisa la Kilutheri)[7] |
---|---|
Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi, mwumba mbingu na dunia. | Namwamini Mungu, BabaMwenyezi, Muumba wa mbingu na nchi. |
na kwa Yesu Kristo, Mwanae pekee, Bwana wetu, aliyetungwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria,
akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu
Siku ya tatu akafufuka kutoka wafu, akapaa mbinguni, ameketi kuume kwa Mungu Baba mwenyezi; kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu. |
Namwamini Yesu Kristo, Mwana wake wa pekee, Bwana wetu, aliyechukiliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Mariamu;
Akateswa zamani za Pontio Pilato, akasulibiwa, akafa, akazikwa, akashuka kuzimu;
|
Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu katoliki, ushirika wa watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili, na uzima wa milele. Amina. | Namwamini Roho Mtakatifu: Kanisa takatifu la Kikristo lililo moja tu[8]; ushirika wa watakatifu. Ondoleo la dhambi, kufufuliwa kwa mwili, na uzima wa milele. Amen. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.