From Wikipedia, the free encyclopedia
Kangaruu (kutoka Kiingereza: kangaroo) ni jina la wanyama mamalia wa spishi mbalimbali walio wenyeji wa Australia. Wote ni wala majani wanaobeba watoto wao wachanga ndani ya pochi ya ngozi iliyopo nje ya mwili juu ya tumbo wakiwa spishi zinazojulikana zaidi ya wanyama wa ngeli ndogo ya marsupialia. Familia ya spishi zao huitwa kwa jina la biolojia Macropodidae yaani wenye miguu mikubwa (kwa Kigiriki makrós (kubwa) na poús (mguu)). Familia hiyo ina spishi takriban 60.
Kangaruu | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Jike la kangaruu kijivu mashariki (Macropus fuliginosus) akiwa na ndama wake kwenye pochi | ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Spishi 4:
| ||||||||||||||||
Kwa matumizi ya kawaida neno hili hutumika kuelezea spishi hii kutoka kwenye familia kubwa hasa wale wa jenasi ya Macropus, kangaruu mwekundu, kangaruu wa kijivu wa magharibi na kangaruu wa kijivu wa mashariki [1]. Kangaruu ni wazawa wa bara la Australia. Jamii nyingine kangaruu wengine wanapatikana pia Australia na New Guinea.
Kangaruu wakubwa wamezoea mabadiliko yaliyosababishwa na kilimo cha kibinadamu katika mazingira yao asilia lakini wale wa spishi za wadogo wengi wapo hatarini. Hawafugwi kwa lolote lakini kangaruu wa mwituni wanawindwa kwa ajili ya nyama, michezo na kulinda malisho ya kondoo na ng'ombe [2] japo kwa vipingamizi. Uwindaji wa kangaroo una faida kubwa kimazingira na kiafya kwa ngombe na kondoo wanaochungwa kwa ajili ya nyama.[3]
Kangaroo ni alama ya taifa ya Australia picha yake inatumika katika ngao ya taifa , kwenye pesa zake na baadhi ya mashirika makubwa ya Australia. Kangaroo ni muhimu sana kwa utamaduni na sura ya taifa ya Australia.
Kuna spishi nne ambazo huonwa kuwa kama ni kangaruu.
Zaidi kuna wanyama wengine wadogo zaidi wanaohusiana kwa ukaribu na kangaruu kwenye familia Macropodidae.
Kwa muda mrefu Ulaya ilimuona kangaroo kama mnyama wa ajabu watu wa mwanzo walisema kuwa kangaroo wanakuwa kama tandala (bila ya pembe); amesimama kama binadamu na anaruka kama chura. Kangaroo wana miguu ya nyuma yenye nguvu, maalumu kwa ajili ya kuruka, mkia mrefu wa nyuma wenye misuli kwa ajili ya balance, na kichwa kidogo, kangaroo jike huwa na mfuko (masupilim) ambamo mtoto humalizia kukua akiwa humo ndani.
Kangaroo ndio wanyama pekee wakubwa wanao jongea kwa kuruka. Mwendo kasi wake wa kuruka kwa kawaida ni km 20 - 25 kwa saa na anaweza kukimbia mpaka kwa kilometa 70 kwa saa kwa umbali mfupi, japo anaweza kukimbia kwa kilometa 40 kwa saa kwa hata kilometa mbili. Mwendo huu umezoeleka kwake kwa sababu yeye si tu kukimbia maalum, lakini mara nyingi hukimbia kutafuta chakula na maji.
Kwa sababu ya wayo zake kubwa hawawezi kutembea vizuri na kwa kasi ndogo. Anatumia mkia wake na miguu ya mbele,kuweka kiegemeo cha miguu mitatu na kasha husogeza miguu yake miwili mikubwa. Kangaruu huishi kwa miaka mine au sita (4-6).
Kangaruu hula nyasi na majani ya vichaka, spishi ndogo za kangaruu hula fungi. Spishi nyingi huchanganyika usiku na hutumia muda mwingi wa mchana kupumzika kivulini, na kutembea kutafuta chakula jioni tulivu, usiku na asubuhi. Kwa sababu ya ulaji wake meno ya kangaroo yamejifanyia meno mengine maalum. Meno yake chonge yanauwezo wa kung’ata nyasi chini kabisa karibu na ardhi na magego yake kwa ajili ya nyasi.mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kama ya chakula usio toa gesi ya methane. Licha ya kuwa na utaratibu wa mfumo wa mmengenyo wa chakula kama wa wanyama wengine wala nyasi, mfano ngombe ambao hutoa kiasi kikubwa cha methane; wakati wa kutoa hewa kangaruu hawatoi nje gesi ya methane. Hewa ya hidrojeni badala ya kuwa methane, hubadilishwa na huwa kemikali ya aseteki, ambayo hutumika kutengeneza nishati zaidi. Wanasayansi wa mimea wanashauku kubwa ya kubainisha bakteria wanaofanya kazi hiyo toka kwa kangaroo mpaka kwa ng'ombe sababu gesi ya methane hutoka kwa ng'ombe. Ng’ombe huchangaia uchafuzi wa hali ya hewa mara 23 zaidi kuliko hewa ya ukaa.
Kangaruu wamejijengea maungo kadhaa yanayo wawezesha kuishi katika makazi yasiyo na rutuba na hali ya hewa yenye kubadilika badilika Bila kutegemewa wakati wa ukame msimu usio wa mvua, Ngamia dume hawazalishi manii, nao kangaroo jike hushika mimba tu kama kuna mvua ya kutosha ya kuzalisha kiasi kikubwa cha majani.
Kuna mahusiano wakati wa kuruka na kupumua kwa kangaroo wakati mguu unatoka ardhini hewa inatoka mapafuni kurusha mguu mbele tayari kwa kutua hujaza tena mapafu kwa hewa kuweka matumizi mazuri ya nishati, uchunguzi umeonesha kuwa zaidi ya nishati inayotumika kuvukia kangaroo huhitaji nishati ndogo sana kama anataka kuvuka sana tofauti na wanyama wengine wanapoongeza kasi ya miendo yao mf. farasi na binadamu
Yai la kangaroo jike huwa ndani ya ovari na hushuka mpaka kwenye uterasi tayari kwa ajili ya kurutubishwa.kijusi hukua kwa haraka sana na kutoka nje baada ya siku 33, kwa kawaida huwa anazaliwa mtoto mmoja tu. Mtoto huyo huwa haoni hana nywele na urefu wa sentimeta chache sana miguu yake ya nyuma huwa inakuwa haijakuwa hivyo hutumia tu miguu ya mbele kujisogeza kwenye mfuko wa mama yake, na huchukua dakika tatu mpaka tano. Akifika ndani ya pochi huanza kunyonya. Baada ya siku 150, mtoto anaweza kutokeza nje kwa mara ya kwanza. Baada ya kuchunguila chungulia nje kwa siku kadhaa na kuona kuwa ni salama. Baada ya hapo hutumia muda wake mwingi kuchungulia nje duniani na baada ya siku 235, hutoka nje ya pochi kwa mara ya mwisho.
Nyama ya kangaroo hupikwa kwa namna mbalimbali. Nyama hii tena ni chakula kwa wakazi asili wa Australia.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.