Remove ads
From Wikipedia, the free encyclopedia
Tenno ni cheo cha mfalme au kaisari wa Japani. Kufuatana na katiba ya nchi yeye ni "ishara wa dola na wa umoja wa taifa".
Tenno wa sasa ni Naruhito (tangu mwaka 2019, alipomrithi baba yake).
Historia ya Japani inamkumbuka tenno wa kwanza kabisa aliyekuwa Jimmu mnamo 660 KK. Wataalamu wengine huwa na shaka lakini wanakubali ya kwamba watawala hao walikuwepo angalau tangu karne ya 5 BK. Hadi karne ya 19 ikulu yao ilikuwa mjini Kyoto, lakini tangu Meiji iko Tokyo.
Nasaba ya watawala wa Japani ni nasaba ya kale zaidi duniani.
Katika historia hiyo ndefu matenno walikuwa na madaraka tofautitofauti. Hata kama walitazamwa kama wakuu wa taifa hali halisi madaraka yao yalikuwa madogo wakati mwingine. Lakini kulikuwa pia na matenno walioamua kabisa juu ya siasa ya nchi kwa mfano Meiji tangu mwaka 1868.
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.