From Wikipedia, the free encyclopedia
Juice ni filamu ya hood yenye maigizo ya uhalifu iliyotolewa mnamo mwaka wa 1992. Ndani yake anakuja rapa Tupac Shakur na Omar Epps wakiwa kama wahusika wakuu wa filamu hii. Wahusika wengine ni pamoja na Jermaine "Huggy" Hopkins, Khalil Kain, Samuel L. Jackson, na kutoa taswira za mwonekano wa baadhi ya wasanii kama vile Queen Latifah, EPMD, Special Ed, Ed Lover, Dr. Dre, Flex Alexander, Fab Five Freddy, na Treach. Filamu imeongozwa na mwanasinematografia Ernest R. Dickerson ambaye ameongoza na kuandika baadhi ya filamu zingine za Hollywood kama vile Surviving the Game na Bulletproof vilevile baadhi ya mifululizo ya vipindi vya televisheni kama vile ER na The Wire.
Juice | |
---|---|
Imeongozwa na | Ernest R. Dickerson |
Imetayarishwa na | David Heyman Gerard Brown James Bigwood Neal H. Moritz Peter Frankfurt Preston L. Holmes Ralph McDaniels |
Imetungwa na | Ernest R. Dickerson Gerard Brown |
Nyota | Omar Epps Tupac Shakur Jermaine "Huggy" Hopkins Khalil Kain Samuel L. Jackson Cindy Herron Queen Latifah Vincent Laresca |
Muziki na | Gary G-Wiz |
Imehaririwa na | Brunilda Torres Sam Pollard |
Imesambazwa na | Paramount Pictures |
Imetolewa tar. | 17 Januari 1992 (U.S.) |
Ina muda wa dk. | 100 min. |
Nchi | U.S.A. |
Lugha | Kiingereza |
Mapato yote ya filamu | $20,146,880[1] |
Filamu inagusa vijana wanne wa Kiafrika-Kiamerika waliokua pamoja mjini Harlem. Inafuatia shughuli za kila siku za wavijana wadogo hao na dhamira zao mbaya zikiwa kama mzaha lakini kadiri siku zinavyoenda suala hilo linazidi kuwa zito zaidi. Pia inalenga hasa michakaliko ya vijana hawa na shida wanazikumbana kila siku kutoka kwa mapolisi, usakamwaji, na matatizo ya kifamilia.
Filamu ilipigiwa katika maeneo ya New York City hasa kwenye maeneo ya Harlem.
Bishop (Shakur), Q (Epps), Raheem (Kain) na Steel (Hopkins), ambao wenye hujiita kama "The Wrecking Crew," vija wanne wa Kiafrika-Kiamerika waliokulia mjini Harlem. Ni kawaida yao kukimbia shule na kutumia siku zao wakiwa katika kituo cha kuchezea game na kupita kwenye maduka ya rekodi na kuiba LP. Siku zote husakamwa na polisi au na kundi la vijana wa kihuni la Kipuerto Rico linaloongozwa na kijana mmoja aitwaye Radames. Siku moja, Bishop aliyekerwa, amechoshwa na masakamo na kuamua kwamba kundi lazima lisonge mbele kwa kufanya mambo makubwa na kujipatia heshima. Lakini Q hana uhakika kama kweli anataka kuendelea kujishughulisha na maisha ya uhalifu. Usiku mmoja wa Jumamosi, ikiwa chini ya ung'ang'anizi wa Bishop, kundi likaamua kuibia kiduka kidogo cha kuuza pombe na chakula cha mtaani. Q ghafula akasita kushiriki kwenye tukio hilo, akiwa hana uhakika kama itafaulu, badala yake akaenda kushiriki kwenye shindano la mkutafuta DJ mkali kitu ambacho alikuwa akiwania kwa miaka mingi. Lakini, lakini kwa uchunguzi uliofanywa na wenzake kundini, akaamua kujiunga. Wakati wanaiba, Bishop mwenye ghadhabu kamtandika risasi ya kichwa Fernando Quiles, mmiliki wa duka lile na hatimaye kufa.
Baada ya vijana kukimbia katika eneo la tukio, wakakusanyika kwenye jumba lililotelekezwa na kuanza kubishana juu ya matukio ya jioni ile. Vijana wakachukizwa na kitendo cha Bishop kumwua Quiles. Hivyo basi Raheem akamtaka Bishop ampatie ile bunduki lakini Bishop hataki kuitoa. Kugombania bunduki ile kumepelekea Bishop kumpiga risasi Raheem. Vijana wengine wakapatwa na mchecheto na kukimbilia jengo lingine. Wakiwa kule, Bishop akatishia kuwauwa wale wengine wawili iwapo watathubutu kusema kile alichokifanya Bishop.
Wale waliobakia wakazungumza na kukubaliana kumuepuka Bishop haraka iwezekanavyo, lakini waliishia kumwona Bishop kwenye mazishi ya Raheem, na kuthubutu hata kukumbatia mama'ke Raheem na kumwahidi atamtafuta aliyemwua Raheem. Kwa kiasi fulani walifanikiwa kwa jaribio lao la kumuepuka Bishop, lakini alishiia kugombana nao mara kwa mara, anawauliza maswali kuhusu uaminifu wao kwake.
Bishop alifanikiwa kumwua mkuu wa wahuni Radames baada ya ugomvi na kuanza kumsingizia Q kama ndiye aliyemwua Quiles, Raheem na Radames. Q akaanza kutafuta msaada na akaashia kuwa na bunduki yake mwenyewe kwa ajili ya usalama wake. Wakati anafanya hili, Bishop akakutana na Steel na kumwongoza kwenye hadi mwisho wa chochoro, ambapo akamtandika risasi, akimshtaki kwa kukosa uaminifu. Hata hivyo, Steel, alikuwa hajafa na kufanikiwa kufika hospitalini na kumtaarifu mpenzi wa Q (Cindy Herron) kwamba amesingiziwa mauaji na Bishop. Amechoshwa na vitu vyote viwili - wasiwasi na na matatizo ya kutumia silaha yaliyompelekea kuwa pale alipo, Q katupa bunduki yake na kuamua kupambana na Bishop akiwa mtupu bila silaha. Q na Bishop mwishowe wakakutana na ugomvi wa kukimbizana ukaanza wakati wa mkutano huu. Q akakimbilia kwenye jengo kubwa halafu anafuatiwa na Bishop, mahali ambapo Q kampora bunduki Bishop na mbio zikaishia juu ya paa refu la ghorofa. Vijana hao walipigana hadi Bishop akaporomoka akawa nje ya shubaka huku mkono mkono mmoja ukishikiliwa na Q. Bishop akamwambia Q asimbwage. Q akahangaikia kumvuta Bishop, lakin kwa bahati mbaya akapata uwezo wake wa kumshika sana kwa mkono na hatimaye Bishop kuanguka na kufa.
Wakati Q anaondoka kule ghorofani, kundi la watu waliokuwa kwenye sherehe wamekusanyika kuangalia nini kilichotokea. Moja kati ya wale watu waliokuwepo kwenye sherehe akamgeukia Q na kusema, "Yo, you got the juice now, man." Q akageuka na kutazama, akatikisa kichwa na kuondoka zake. Filamu inaishia kuonesha marafiki wote wanne wakati wapo kwenye kipindi cha furaha kubwa.
Mwigizaji | Uhusika |
---|---|
Tupac Shakur | Roland Bishop |
Khalil Kain | Raheem Porter |
Omar Epps | Quincy 'Q' Powell |
Jermaine 'Huggy' Hopkins | Eric 'Steel' Thurman |
Samuel L. Jackson | Trip |
Queen Latifah | Ruffhouse M.C. |
Bruklin Harris | Keesha |
Rotten Tomatoes wameipa filamu 82% ya "viwango safi kabisa".[2]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.