From Wikipedia, the free encyclopedia
James Polin Gray (alizaliwa Februari 14, 1945) ni mwanasheria na mwandishi kutoka nchini Marekani. Alikuwa hakimu msimamizi wa Mahakama ya Juu ya Kaunti ya Orange, California. Gray alikuwa makamu wa rais wa Chama cha Libertarian mwaka 2012, na pia mgombeaji wa chama hicho mnamo mwaka 2004 katika Seneti ya Marekani huko California.Ni mwandishi wa vitabu na pia muandishi wa tamthilia na ni mkosoaji mkubwa wa sheria za dawa za nchini marekani.
Gray ni Mzaliwa wa Washington, D.C. na alilelewa katika eneo la Los Angeles, huko California, Gray alipata digrii yake ya shahada ya kwanza kutoka Chuo Kikuu cha California, Los Angeles mnamo mwaka 1966, kisha akafundisha katika Peace Corps huko Kosta Rika. Gray alirudi California na kupata digrii ya Udaktari wa sheria kutoka Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Southern California mnamo mwaka 1971.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.