From Wikipedia, the free encyclopedia
Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kikazakhi ilikuwa kati ya jamhuri 15 wanachama wa Umoja wa Kisovyeti hadi mwaka 1991. Jina lake liliandikwa kwa alfabeti ya Kikirili katika lugha ya Kikazakhi: "Қазақ Советтік Социалистік Республикасы" (Kasak Sovyettik Sotsialistik Respublikasi) au ya Kirusi: "Казахская Советская Социалистическая Республика" (Kazakhskaya Sovyetskaya Sotsialisticheskaya Respublika).
Jamhuri ya Kikazakhi ndani ya Umoja wa Kisoveti | |
Wito la Umoja wa Kisovyeti: Барлық елдердің пролетарлары, бірігіңдер! | |
Lugha rasmi | hali halisi Kikazakhi na Kirusi |
Mji Mkuu | Alma-Ata (leo: Almaty) |
Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Kazakhstan | Nursultan Nasarbajew |
Kuanzishwa kama Jamhuri - Jamhuri ndani ya Umoja wa Kisoveti - kufutwa |
26 Agosti 1920 30 Desemba 1922 16 Desemba 1991 |
Eneo
- % maji |
2,717,300 km² (wa pili katika Umoja wa Kisovyeti) 1.7% |
Wakazi | 16,711,900 (sensa 1989) |
Msongamano | 6.1/km² |
Pesa | Rubel (рубль) |
Kanda za Wakati | UTC +4 hadi +6 |
Yenye eneo la km² 2,717,300 ilikuwa jamhuri kubwa ya pili ndani ya Umoja wa Kisovyeti baada ya Urusi.
Mji mkuu ulikuwa Alma-Ata inayoitwa leo Almaty.
Tangu Desemba 1991 imekuwa nchi huru ya Kazakhstan katika Asia ya Kati.
Jina la nchi limetokana na Wakazakhi ambao ni taifa la watu wanaotumia Kikazakhi, mojawapo ya lugha za Kiturki.
Eneo liliwahi kuwa sehemu ya milki mbalimbali lakini tangu karne ya 15 Wakazakhi walijaribu kuungana mara kadhaa bila mafanikio ya kudumu.
Tangu karne ya 17 milki ya Urusi ilianza kuenea katika Asia ya Kati na hadi mwaka 1865 eneo lote la Kazakhstan lilitawaliwa na Urusi.
Baada ya mapinduzi ya Urusi ya 1917 Wakomunisti walichukua nafasi ya Matsar wa awali wakafanya nchi kuwa jamhuri yenye kiwango cha kujitawala ndani ya Jamhuri ya Kirusi ya Umoja wa Kisovyeti.
Mwaka 1936 nchi ilipewa cheo cha jamhuri kamili ndani ya Umoja wa Kisovyeti. Katika miaka iliyofuata Warusi na watu wa mataifa mengine ya Umoja huo walihamishiwa nchini hadi Wakazakhi kubaki kuwa chini ya nusu ya wakazi wote.
Miaka 1990/1991 wakati wa kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti jamhuri ilijiondoa polepole. Kiongozi wa chama cha kikomunisti cha Kazakhstan Nursultan Nasarbajew alitangaza uhuru wa nchi na kuwa rais wa kwanza akiendelea kutawala kama awali.
Wakomunisti walifanya jitihada kubwa kuchimba madini na kuanzisha viwanda pamoja na kupanua kilimo. Miradi mikubwa ya kumwagilia ardhi yabisi yaliwezesha mavuno makubwa lakini yalisababisha pia kukauka kwa ziwa Aral.
Umoja wa Kisovyeti ulijenga uwanja wa roketi wa Baikonur uliokuwa kituo kikuu cha kurusha vyombo vya angani.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.