From Wikipedia, the free encyclopedia
Jaipur ni mji mkuu wa jimbo la Rajastan nchini Uhindi. Mnamo mwaka wa 2011, karibu watu milioni tatu waliishi hapo. Iko mnamo km 300 kusini magharibi kwa Delhi na takriban km 200 magharibi kwa Agra.
Kuna viwanda mbalimbali katika jiji hilo, ambalo pia ni kitovu cha kiutamaduni kinachopokea watalii wengi.
Paoneaanga pa kale pa Jantar Mantar, kitovu cha kihistoria cha Jaipur na Ngome ya Amer vimepokewa katika orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO. Jaipur ina chuo kikuu.
Ni pia kitovu cha usafiri ambako njia za reli na barabara muhimu zinakutana.
Ni mmoja kati ya miji ya Uhindi ambako uhaba wa maji ya kunywa ni mkali; kufuatana na makadirio maji yanaweza kwisha kabisa mnamo mwaka 2020.[1]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.