From Wikipedia, the free encyclopedia
Injini ya dizeli ni injini ya mwako ndani ambamo kuwaka kwa mafuta husababishwa na joto la juu linalotokana na kugandamiza hewa ndani ya silinda zake. Hii ni tofauti na injini zinazowasha mchanganyiko wa mafuta na hewa kwa njia ya heche za umeme, kama vile injini ya petroli au injini ya gesi (gesi asilia au gesi ya LPG). Injini ya dizeli ilibuniwa na mhandisi Mjerumani Rudolf Diesel katika karne ya 19.
Injini ya diseli inahitaji kutengeneza shinikizo kali ndani yake hivyo ni imara na nzito zaidi kuliko injini ya petroli. Hapo awali ilitumika kama mbadala wa injini za mvuke zilizosimama . Tangu miaka ya 1910, zilitumika pia katika manowari na meli. Iliendelea kutumika katika vichwa vya treni, mabasi, malori, matrekta na majenereta ya kuzalisha umeme. Katika miaka ya nyuma mahandisi walifaulu kutengeneza pia injini ndogo za diseli zinazotumiwa katika magari madogo.
Tangu miaka ya 1970, matumizi ya injini za dizeli katika magari makubwa ya barabarani na nje ya barabara nchini Marekani yameongezeka. Kulingana na Konrad Reif (2012), nusu ya magari madogo katika Umoja wa Ulaya ni magari ya dizeli.
Injini kubwa zaidi za dizeli zinazotumiwa duniani zina silinda 14 zinazotumiwa kwenye meli kubwa.
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.