Injini ya mvuke
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Injini ya mvuke ni injini inayotumia nguvu ya mvuke kwa kufanya kazi. Nguvu ya mvuke ni nishati ya joto iliyomo ndani yake. Nishati hii inabadilishwa kuwa mwendo.
Ndani ya mashine maji hupashwa moto kuyageukia kuwa mvuke. Mvuke unaingizwa katika silinda ambako unasukuma pistoni ndani yake. Mwendo wa pistoni unabadilishwa kuwa mwendo wa kuzunguka kupitia fitokombo.
Injini za kwanza za mvuke zilitengenezwa kwa kuendesha pampu za kuvuta maji kwenye migodi ya makaa huko Uingereza. Kuanzia miaka ya 1780 mafundi waliongeza gia na fitokombo na hivyo injini ya mvuke ilitumiwa hata viwandani kuendesha mashine mbalimbali zilizowahi kutumia awali nguvu ya wanadamu au ya wanyama. Mhandisi James Watt anakumbukwa kwa uboreshaji wa injini za kwanza.
Injini ya mvuke ilikuwa uti wa mgongo wa upanuzi wa viwanda na mapinduzi ya viwanda yaliyoendelea kubadilisha maisha na jamii kwanza huko Uingereza, halafu Ulaya na kote duniani.
Injini za mvuke ziliendelea kusukuma magari ya kwanza ama barabarani au kwenye reli. Jina la "gari la moshi" bado linakumbuka asili hii hata kama leo injini za reli ni za diseli au umeme si tena mvuke. Siku hizi injini za mvuke karibu zimepotea kiwandani na pia kwenye magari. Lakini kutokana na uhaba wa mafuta ya petroli unaotarajiwa kwa miaka ujao kuna majarabio mapya kutengeneza magari yanayoendeshwa tena kwa injini za kisasa za mvuke.
Kwa jumla kuna bado matumizi ya aina ya injini ya mvuke katika vituo vya umeme. Mara nyingi umeme hutengenezwa kwa kuchemsha maji ama kwa mafuta au makaa au nyuklia na kutumia nishati ya joto ndani ya mvuke wa maji kuzungusha tabo au jenereta.
- Injini ya mvuke kwenye makumbusho ya Deutsches Museum (München)
- Injini ya mvuke iliyovuta eleveta katika mgodi
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Injini ya mvuke kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Remove ads
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.
Remove ads