Ziwa Great Slave (kwa Kifaransa: Grand lac des Esclaves; kwa Kiingereza: Great Slave Lake) ni ziwa la pili kwa ukubwa katika maeneo ya Northwest Territories ya Kanada. Ni ziwa lenye kina kirefu zaidi katika Amerika Kaskazini likifikia mita 614 [1] na ziwa kubwa la tisa duniani. Urefu wake ni km 480 likiwa na upana wa km 19 hadi 109, hivyo kuwa na eneo la km2 27,200.

Ukweli wa haraka
Ziwa Great Slave
Thumb
Ufuko wa mashariki
Nchi zinazopakana Kanada, jimbo la Northwest_Territories
Eneo la maji km2 27,200
Kina cha chini m 614
Mito inayoingia Mito ya Hay, Slave, Taltson, Lockhart, Yellowknife
Mito inayotoka Mto Mackenzie
Kimo cha uso wa maji
juu ya UB
m 156
Funga

Jina linatokana na neno la utani la Maindio wa Cree kwa maadui wao waliokalia sehemu ya ziwa. Waliwaita "watumwa" na jina hili lilitafsiriwa na Wafaransa wa kwanza waliofanya biashara na Wacree na kuingizwa katika ramani zao wakiandika "Lac des Esclaves" (ziwa la Watumwa, walishika pia "mto wa watumwa"). Umbo hili la Kifaransa lilitafsiriwa baadaye kwa Kiingereza "Slave Lake", ilhali kuna "Great Slave Lake" na "Lesser Slave Lake", pia "Slave River".

Miji kwenye ziwa ni pamoja na: Yellowknife, Hay River, Behchoko, Fort Resolution, Lutselk'e, Hay River Reserve, Dettah na N'Dilo.

Picha

Marejeo

Tovuti za Nje

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.