From Wikipedia, the free encyclopedia
Kunguni-chura ni wadudu wadogo wa familia Gelastocoridae katika oda ya chini Nepomorpha ya oda Hemiptera wanaofanana na vyura wadogo kwa sura na tabia. Kuna spishi takriban 120 duniani kote, isipokuwa Ulaya, lakini spishi 1 tu barani Afrika[1].
Kunguni-chura | ||||||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Nerthria sp. nchini Australia | ||||||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||||||||
Nusufamilia 2; jenasi 3, 1 katika Afrika ya Mashariki:
| ||||||||||||||||||||||||
Kunguni-chura wana urefu wa mm 6-15. Mwili wao ni imara na una umbo la duaradufu .Miguu yao ya mbele ni imara na inatumiwa kukamata mbuawa. Miguu ya kati na ya nyuma inatumiwa kwa kuruka juu ya mbuawa[2]. Sehemu za kinywa ni imara na kama sindano. Kwa kawaida wadudu hao hawana mabawa ya nyuma na kwa hivyo hawawezi kuruka angani. Mara nyingi mabawa ya mbele yameunganishwa. Vipapasio vimefichwa katika mifuo ya uso. Rangi ni kama kamafleji na hata wanaweza kubadilisha rangi ili kuilingana na mazingira yao.
Wadudu hao huishi kando ya maji kwa kawaida, lakini spishi kadhaa zimepatikana mbali na maji. Huwinda vertebrata wadogo kwa kuruka juu yao ambao wanawatoboa kwa kinywa chao na kufyonza yaliyomo.
Mayai hutagwa kwenye mchanga[3]. Tunutu (lava) hujifunika kwa tabaka la chembe za mchanga ili kutoonekana dhidi ya nyuma[4].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.