From Wikipedia, the free encyclopedia
Gaetano wa Thiene (Vicenza, 1 Oktoba 1480 – Napoli, 7 Agosti 1547), alikuwa padri wa Italia ambaye alichangia sana uamsho wa Kanisa wakati wa Urekebisho wa Kikatoliki hasa kwa njia ya aina mpya ya utawa aliyoianzisha, maarufu kwa jina la Wateatini, aliowaachia jukumu la kufuata mtindo wa maisha ya Mitume wa Yesu. Kwa shirika hilo alifungua njia kwa mashirika mengine kama la Wajesuiti, la Wabarnaba na la Wasomaski.
Huko Napoli alijitosa katika matendo ya huruma, hasa kwa ajili ya waliopatwa na magonjwa wasiotibika, na kuhamasisha vyama kwa ajili ya malezi ya Kikristo ya walei [1].
Alitangazwa na Papa Urban VIII kuwa mwenye heri tarehe 8 Oktoba 1629, halafu Papa Klementi X alimtangaza mtakatifu tarehe 12 Aprili 1671.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.