Fransisko Jaccard, M.E.P. (1799-1838) alikuwa padri wa Ufaransa mmisionari huko Vietnam. Chini ya kaisari wa huko, Minh Mang, alifungwa, akateswa akanyongwa pamoja na Thomas Thien Tran kwa ajili ya Kristo[1].

Ni mmojawapo kati ya Wakristo wafiadini wa Vietnam waliouawa kwa ajili ya imani yao huko Vietnam katika karne ya 17, 18 na 19 (16251886).

Wanatajwa pia kama Watakatifu Andrea Dũng-Lạc na wenzake 116.

Kwa nyakati tofauti, Papa Leo XIII, Papa Pius X na Papa Pius XII waliwatangaza kuwa wenye heri, halafu Papa Yohane Paulo II aliwaunganisha katika kuwafanya watakatifu wafiadini tarehe 19 Juni 1988.

Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 24 Novemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 21 Septemba[2].

Tazama pia

Marejeo

  • Les Missions Etrangères. Trois siecles et demi d'histoire et d'aventure en Asie Editions Perrin, 2008, ISBN 978-2-262-02571-7
  • "St. Andrew Dung-Lac & Martyrs", by Father Robert F. McNamara, Saints Alive and All God's Children Copyright 1980-2010 Rev. Robert F. McNamara and St. Thomas the Apostle Church.
  • "Vietnamese Martyr Teaches Quiet Lessons", By Judy Ball, An AmericanCatholic.org Web Site from the Franciscans and St. Anthony Messenger Press.

Tanbihi

Viungo vya nje

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.