Silaha za moto (kwa Kiing. firearm) ni vifaa vinavyorusha risasi dhidi ya shabaha kupitia kasiba (mtutu) yake kwa nguvu ya gesi inayopanuka kutokana na kuchomeka ghafla kwa baruti ndani ya silaha yenyewe.

Thumb
Moto unaonekana mbele ya mdomo wa bastola wakati wa kufyatua risasi.
Thumb
Moto kutoka mdomo wa mzinga wa kifaru ni mkubwa.

Kutokana na mlipuko wa baruti ndani ya silaha moto huonekana mdomoni mwa silaha kila safari risasi imefyatuliwa.

Kati ya silaha za moto kuna kwa mfano:

  • gobori, pia korofindo (silaha za moto za kwanza; baruti na risasi zinaingizwa kupitia mdomo wa kasiba; ing. musket)
  • bunduki (silaha ndefu ya moto inayoshikwa kwa mikono; baruti na risasi zinaunganishwa kwa umbo la ramia inayoruhusu kufyatulia haraka kushinda kwa gobori, ing. rifle)
  • bastola (bunduki fupi inayoweza kushikwa kwa mkono mmoja, ing. handgun, pistol, revolver)
  • bombomu (bunduki inayoweza kufyatua risasi nyingi kwa muda mfupi, ing. machine gun)
  • mzinga (kifaa kikubwa kama bunduki kinachofyatua risasi kwa umbali mkubwa; huwekwa juu ya magurudumu, au hufungwa kwenye kifaru au manowari, ing. cannon, artillery gun)

Kuna pia silaha zinazorusha risasi kupitia kasiba ambazo si silaha za moto, kwa mfano bunduki ya hewa.

Wataalamu hufanyia utafiti silaha mpya zinazorusha risasi kwa kutumia nguvu ya sumakuumeme.

Viungo vya nje

Ukweli wa haraka
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Funga

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.