Filipo II wa Masedonia[1] (kwa Kigiriki: Φίλιππος Β΄ ὁ Μακεδών, Phílippos II ho Makedṓn; 382 KK336 KK) alikuwa mfalme wa Masedonia katika Ugiriki wa Kale kuanzia mwaka 359 KK hadi alipouawa.

Thumb
Sanamu ya Filipo II.

Mnamo 500 KK kulikuwako ufalme ulioitwa Masedonia ambao ulihesabiwa kama sehemu ya utamaduni wa Ugiriki wa kale na wafalme waliruhusiwa kwenye michezo ya Olimpiki ya madola ya Wagiriki.

Pamoja na sehemu nyingi za Ugiriki ufalme huo ulipaswa kukubali ubwana wa Milki ya Uajemi, lakini Filipo alifaulu kuurudisha uhuru akaendelea kuifanya Masedonia kuwa dola kiongozi kati ya madola madogo ya Ugiriki.

Mwanawe Aleksanda Mkuu aliimarisha utawala wake juu ya Wagiriki wengine na kushambulia Milki ya Uajemi na hatimaye kuivamia na kuishinda kwa jeshi kutoka sehemu zote za Ugiriki.

Tanbihi

Viungo vya nje

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.