Felisi wa Como

From Wikipedia, the free encyclopedia

Felisi wa Como (alifariki 8 Oktoba 391 BK) anakumbukwa kama askofu wa kwanza wa Como (Italia Kaskazini).

Rafiki wa Ambrosi wa Milano, alisifiwa naye kwa umisionari wake akapewa naye upadrisho mwaka 379[1] na daraja ya uaskofu kwa ajili ya Como tarehe 1 Novemba 386[2] katika juhudi za kukamilisha uenezi wa Ukristo kote Italia baada ya Kaisari Theodosi I kuufanya dini rasmi ya Dola la Roma.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[3] au tarehe 1 Julai.[4]

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.