From Wikipedia, the free encyclopedia
Dubni (kwa Kiingereza: Dubnium) ni elementi sintetiki yenye namba atomia 105 kwenye mfumo radidia, uzani atomia ni takriban 262. Alama yake ni Db.
Dubni (dubnium) | |
---|---|
Jina la Elementi | Dubni (dubnium) |
Alama | Db |
Namba atomia | 105 |
Mfululizo safu | Metali ya mpito |
Uzani atomia | 262.0 |
Valensi | 2, 8, 18, 32, 32, 11, 2 |
Densiti | 29.3 g/cm³ (kadirio) |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Asilimia za ganda la dunia | 0 % (elementi sintetiki) |
Hali maada | inaaminiwa ni mango |
Mengineyo | tamburania, nururifu |
Baada ya kugunduliwa katika maabara iliitwa majina tofauti kama vile eka-tantalum, hahnium na unnilpentium lakini hatimaye jina likawa Dubni kwa kumbukumbu ya mji wa Urusi wa Dubna ambako iligunduliwa.
Ni elementi nururifu sana isiyopatikana kiasili. Ni elementi sintetiki au tamburania yaani haipatikani kiasili. Sababu yake ni kwamba nusumaisha ya isotopi zake ni fupi mno. 268Db (isotopi thabiti zaidi) ina nusumaisha ya masaa 28[1].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.