From Wikipedia, the free encyclopedia
Titus Flavius Domitianus (24 Oktoba 51 – 18 Septemba 96) alikuwa Kaizari wa Dola la Roma kuanzia 14 Septemba, 81 hadi kifo chake. Alimfuata kaka yake Titus.
Domitiano aliimarisha utaratibu wa Dola. Alijitahidi kutafuta maafisa wenye uwezo nje ya familia ya wakubwa wa Senati hivyo alikuta upinzani aliokandamiza vikali.
Alijitahidi kuimarisha pia dini ya Kiroma. Waandishi Wakristo kama Eusebi waliandika karne mbili baadaye kwamba alitesa Wayahudi na Wakristo waliokataa kuabudu miungu ya Roma lakini wataalamu wa siku hizi hawawezi kuthibitisha habari hiyo[1].
Vitabu vya Ufunuo wa Yohane pamoja na waraka wa kwanza wa Klementi viliandikwa wakati ule.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.