From Wikipedia, the free encyclopedia
Dimenshia ni kategoria pana ya magonjwa ya ubongo yanayosababisha upunguaji wa muda mrefu na mara kwa mara wa polepole katika uwezo wa kufikiria na kukumbuka kiasi kwamba utendakazi wa kawaida wa mtu unaathiriwa.[1] Dalili zingine zinazotokea sana ni matatizo ya kihisia, matatizo ya lugha, na upungufu katika motisha.[1][2] Ufahamu wa mtu hauathiriwi.[1] Ili utambuzi uweze kufaulu, ni lazima kuwe na mabadiliko kutoka kwa utendakazi wa kawaida wa akili ya mtu na upungufu mkubwa kuliko utokanao na kuzeeka.[1][3] Magonjwa haya pia yana athari kubwa kwa watunzaji wa mtu.[1]
Aina inayopatikana sana ya dimenshia ni ugonjwa wa Alzheimer unaochangia asilimia 50 hadi 70 ya visa. Aina zingine zinazopatikana sana ni dimenshia ya mishipa (asilimia 25), dimenshia ya Lewy body (asilimia 15), na dimenshia ya muda ya upande wa mbele.[1][2] Visababishi visivyopatikana sana ni hidrosefalasi ya shinikizo la kawaida, ugonjwa wa Parkinson, kaswende, na ugonjwa wa Creutzfeldt–Jakob miongoni mwa vingine.[4] Zaidi ya aina moja ya dimenshia zinaweza kuwa kwa mtu mmoja.[1] Kiasi kidogo cha visa huathiri familia.[5] Katika DSM-5, dimenshia iliainishwa upya kama tatizo la neva tambuzi, na viwango tofauti vya ukali.[6] Utambuzi hutegemea historia ya maradhi hayo na uchunguzi wa utambuzi kwa picha za mwanga wa kitabibu na vipimo vya damu kuondoa visababishi vingine vinavyoweza kuwepo.[7] Uchunguzi mdogo wa hali ya akili ni kipimo cha ufahamu kinachotumika sana.[2] Juhudi za kuzuia dimenshia ni kujaribu kupunguza visababishi vya hatari kama vile shinikizo la juu la damu, kuvuta, kisukari na unene.[1] Uchujaji umma kwa jumla kwa ugonjwa huu haupendekezwi.[8]
Hakuna tiba ya dimenshia.[1] vizuio vya Kolinisteresi kama vile donepezil hutumiwa mara kwa mara na vinaweza kusaidia katika ugonjwa mdogo ili kupunguza.[9][10][11] Faida ya jumla, hata hivyo, inaweza kuwa ndogo.[11][12] Kwa watu walio na dimenshia na wale wanaowatunza, hatua nyingi zinaweza kuboresha maisha yao.[1] Tatuzi za kiufahamu za kitabia zinaweza kuwa bora.[1] Kuelimisha na kutoa msaada wa kihisia kwa mtunzaji ni muhimu.[1] Programu za mazoezi ni muhimu kulingana na shughuli za maisha ya kawaida na huboresha matokeo.[13] Matibabu ya matatizo ya kitabia au saikosisi kutokana na dimenshia kwa vizuia saikosisi hutumika sana lakini hayapendekezwi kutokana na suala kuwa huwa na faida ndogo na hatari zaidi ya kifo.[14][15]
Ulimwenguni, dimenshia huathiri watu milioni 36.[1] Takribani asilimia 10 ya watu hupata ugonjwa huu wakati fulani maishani mwao.[5] Hupatikana sana umri unapoongezeka.[16] Takribani asilimia 3 ya watu wa umri wa kati ya miaka 65–74 wana dimenshia, asilimia 19 kati ya umri wa miaka 75 na 84 na karibu nusu ya walio na umri wa miaka 85.[17] Katika mwaka wa 2013 dimenshia ilisababisha takribani vifo milioni 1.7, juu kutoka milioni 0.8 katika mwaka wa 1990.[18] Watu wengi wanapoishi zaidi, dimenshia inaendelea kupatikana sana kwa watu wote.[16] Kwa watu wa umri mahususi; hata hivyo, huenda ikawa kuwa unapungua, angalau katika nchi zilizostawi, kutokana na kupungua kwa visababishi vya hatari.[16] Ni mojawapo ya visababishi vikuu vya ulemavu miongoni mwa wazee.[2] Inaaminika kusababisha gharama za kiuchumi za dola bilioni 604 kila mwaka.[1] watu walio na dimenshia mara nyingi huwa na vizuizi vya kimwili au kikemikali kwa kiwango kikubwa kupita kiasi, na kuibua masuala ya haki za kibinadamu.[1] Shutuma za kijamii dhidi ya waathiriwa hutokea sana.ref name=BMJ2009/>
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.