From Wikipedia, the free encyclopedia
Dawa ya kibiolojia ni dawa ya kudhibiti viumbehai wasumbufu au waharibifu ambayo ina viambato viasilia, k.m. vidubini au misindiko ya mimea. Dawa hizi huunda sehemu ya udhibiti wa kibiolojia pamoja na kuachia kwa wadudu wa kidusia au vidusia vyingine.
Fasiri zinatofautiana kati ya nchi, k.m.:
Kwa kawaida zinategenezwa kwa kukuza na kukusanya vidubini vinavyotokea uasiliani, labda pamoja na vifundiro vya metaboli vyao, k.m. bakteria, virusi, kuvu na protozoa. Nematodi hushirikishwa katika orodha hii ijapokuwa si vidubini kwa kweli. Dawa hizi zinachukuliwa mara nyingi kama visehemu shiriki vya miradi ya mchanganyiko wa udhibiti wa viharibifu (Kiing.: integrated pest management) na zinatumika zaidi na zaidi badala ya dawa za kikemikali[3].
Kuna madaraja makubwa matatu ya dawa za kibiolojia:
Bacillus thuringiensis (Bt) anasababisha magonjwa katika vipepeo, mbu na mende-vibyongo. Dawa zenye Bt zinaitwa dawa za vidukini kwa kawaida lakini hii siyo sahihi kabisa kwa sababu wingi wa dawa hizi hazina bakteria hai ndani yao lakini fuwele za sumu zao tu. Jeni zilizo na kodi ya kutengeneza sumu hizi zimeingizwa katika mimea ipandwayo, k.m. mpamba, muhindi, kiazi cha kizungu na soya. Kwa hivyo mimea hii inaweza kuua viwavi na lava wa mende-vibyongo bila haja ya kupulizia dawa. Ingawa dawa zenye Bt na mimea yenye jeni za sumu za Bt hazina hatari kwa viumbehai vingine kuliko dawa za kikemikali, mgusano uliorudia au wa muda mrefu na sumu za Bt unaweza kusababisha mabadiliko ya kihistopatolojia katika ini na mafigo ya mamalia[8].
Dawa nyingi za vidubini zina kuvu viuawadudu ndani yao, kama spishi za Metarhizium, Beauveria, Isaria na Lecanicillium. Dawa hizi hazina haja ya kumezwa kwa sababu kuvu hizi zinapenya kiunzi nje cha wadudu. Kuna spishi nyingi za virusi zinazotumika katika dawa za vidubini, lakini ni lazima dawa hizi zimezwe. Kinyume na virusi na kuvu nematodi viuawadudu, kama spishi za Steinernema na Heterorhabditis, huingia wenyewe kupitia tundu yoyote ya kiwiliwili (kinywa, mkundu, spirakulo n.k.) lakini spishi kadhaa zinaweza kupenya kiunzi nje. Dawa za kudhibiti magonjwa ya mimea zina kuvu kama spishi za Trichoderma au bakteria kama spishi za Bacillus (B. subtilis hasa). Mwishowe kuna dawa za kiuamagugu zilizo na kuvu kama spishi za kuvu-kutu.
Dawa za kibiokemikali zinaweza kuwa na misindiko ya mimea iliyo na alkaloidi, terpenoidi na fenoli ndani yao. Mfano unaojulikana sana ni mafuta ya mwarobaini (Kiing.: neem oil). Dawa nyingine zina vifundiro vya kuchachuka kama Spinosad. Hata wadudu wanatengeneza molekuli ambayo zinaweza kutumika kama dawa, mahususi feromoni. Molekuli hizi haziui lakini zinatafiri kupandana kwa wadudu.
Kwa kawaida dawa za kibiolojia hutumika kwa njia sawa kama dawa za kikemikali lakini namna za matendo ni tofauti na bila hatari kwa mazingira. Ili kufanya kazi vizuri ni lazima dawa hizi zichanganywe na viambato na vizimuo sadifu[9] na njia sadifu za kupulizia zitumike[10][11]. Hata hivyo, mara nyingi hali ya hewa ni ya maana, k.m. unyevuanga mkubwa.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.