From Wikipedia, the free encyclopedia
Ndoo (pia: Dalu) ni kundinyota la zodiaki linalojulikana kimataifa kwa jina lake la kimagharibi la Aquarius[1]. Ni moja ya kundinyota zinazotambuliwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia [2]
Nyota za Ndoo huwa haziko pamoja kihalisi lakini zinaonekana tu vile kutoka duniani. Kwa uhalisi kuna umbali mkubwa kati yao, kama ziko mbali au jirani nasi. Kwa hiyo kundinyota "Ndoo" linaonyesha eneo la angani jinsi tunavyoiona kutoka Duniani.
Kundinyota hili linajulikana kwa jina la Dalu kwa miaka mingi kwa mabaharia Waswahili walioitumia kutafuta njia baharini wakati wa usiku.[3]
Jina asilia la Dalu linatokana na Kiarabu دلو dalu ambalo linamaanisha "ndoo ya kubebea maji". Jina hili lilipokelewa na Waarabu kutoka kwa Wagiriki wa Kale waliosema Ὑδροχόος hidro-kho-os "mwagiliaji maji" na hao walipokea kundinyota hili kutoka kwa Wababeli.
Katika unajimu wa kisasa katika Afrika ya Mashariki jina "Dalu" limesahauliwa ikiwa kundinyota linaitwa kutokana na ishara yake tu "Ndoo".
Ndoo iko angani kwenye mstari wa ekliptiki kati ya Mbuzi au Jadi (en:Capricornus) na Hutu (en:Pisces).
Kuna nyota nyingi katika eneo la kundinyota hili lakini zote si angavu sana. Nyota angavu zaidi ni Beta Aquarii ambayo ni nyota jitu kubwa njano yenye mwangaza unaoonekana wa 2.9.
Nyota kadhaa zilitambuliwa kuwa na mifumo ya sayari kwa mfano nyota Gliese 876[4] .
Jina la (Bayer) |
Namba ya Flamsteed |
Jina (Ukia) |
Mwangaza unaoonekana |
Umbali (miakanuru) |
Aina ya spektra | |
---|---|---|---|---|---|---|
β | 22 | Sadalsuud | 2,90 | -3,5 | 610 | G0 Ib |
α | 34 | Sadalmelik | 2,95 | -3,9 | 760 | G2 Ib |
δ | 76 | Skat | 3,27 | -0,2 | 160 | A3 V |
γ | 48 | Sadachbia | 3,86 | 0,44 | 158 | A0 |
λ | 73 | 3,73 | -1,7 | 390 | M2 III | |
ε | 2 | Albali | 3,78 | -0,46 | 230 | A1 V |
η | 62 | 4,04 | 0,29 | 184 | B9 IV | |
θ | 43 | Ancha | 4,17 | 0,33 | 191 |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.