Teleka au barawai ni ndege wa familia Apodidae. Ndege hawa ni wadogo wenye mabawa marefu kwa umbo wa mundu. Rangi yao ni kahawia au kijivu na mara nyingi kiuno, koo na/au tumbo ni nyeupe. Teleka hupitisha takriban maisha yao yote angani wakikamata wadudu. Kwa hivyo ndege hawa hawawezi kutembea vizuri. Zamani watu walifikiri kwamba teleka hawana miguu, wakawapatia jina “apus” kutoka Kiyunani α = bila na πους = mguu. Hunywa pia wakiruka, lakini hulala wakishika nyuso ya wima.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Teleka |
Teleka mweusi |
Uainishaji wa kisayansi |
Himaya: |
Animalia (Wanyama)
|
Faila: |
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
|
Nusufaila: |
Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
|
Ngeli: |
Aves (Ndege)
|
Oda: |
Apodiformes (Ndege kama teleka)
|
Familia: |
Apodidae (Teleka) Hartert, 1897 |
|
Ngazi za chini |
Nusufamilia 2 na enasi 29:
- Apodinae Hartert, 1897
- Aerodramus Linnaeus, 1758
- Aeronautes Hartert, 1892
- Apus Swainson, 1832
- Chaetura >Wagler, 1832
- Collocalia >G.R. Gray, 1840
- Cypsiurus G.R. Gray, 1840
- Hirundapus Cassin, 1851
- Hydrochous Brooke, 1970
- Mearnsia Ridgway, 1911
- Neafrapus P.L. Sclater, 1866
- Panyptila Cabanis, 1847
- Rhaphidura Bonaparte, 1857
- Schoutedenapus Wagler, 1832
- Tachornis Gosse, 1847
- Tachymarptis Ridgway, 1880
- Telacanthura P.L. Sclater, 1861
- Zoonavena W. Miller, 1915
- Cypseloidinae Bonaparte, 1838
- Cypseloides Streubel, 1848
- Streptoprocne Oberholser, 1906
|
Funga
Teleka hujenga tago lao kwa vitu mbalimbali (vitawi, maua, majani, nyuzi, manyoya, wadudu) ambavyo vinagundishwa pamoja na mate. Matago ya spishi nyingine yamejengwa kwa mate pekee na haya yalika, huko Uchina hasa. Jike huyataga mayai 1-4.
- Aerodramus elaphrus, Teleka Mdogo wa Shelisheli (Seychelles Swiftlet)
- Aerodramus francicus, Teleka Mdogo wa Maskarena (Mascarene Swiftlet)
- Apus affinis, Teleka Mdogo (Little Swift)
- Apus alexandri, Teleka wa Kepuvede (Cape Verde au Alexander's Swift)
- Apus apus, Teleka wa Ulaya (Common Swift)
- Apus balstoni, Teleka wa Madagaska (Madagascar Swift)
- Apus barbatus, Teleka Mweusi (African Black Swift)
- Apus batesi, Teleka wa Bates (Bates's Swift)
- Apus berliozi, Teleka Somali (Forbes-Watson's Swift)
- Apus bradfieldi, Teleka wa Bradfield (Bradfield's Swift)
- Apus caffer, Teleka Kiuno-cheupe (White-rumped Swift)
- Apus horus, Teleka Koo-kijivu (Horus Swift)
- Apus niansae, Teleka wa Nyanza (Nyanza Swift)
- Apus pallidus, Teleka-majabali (Pallid Swift)
- Apus sladeniae, Teleka wa Fernando Po (Fernando Po Swift)
- Apus unicolor, Teleka Bilachoro (Plain Swift)
- Cypsiurus parvus, Teleka-mitende au Teleka Mkia-mrefu (African Palm Swift)
- Neafrapus boehmi, Teleka-mkiasindano wa Böhm (Böhm's Spinetail)
- Neafrapus cassini, Teleka-mkiasindano wa Cassin (Cassin's Spinetail)
- Rhaphidura sabini, Teleka-mkiasindano wa Sabine Sabine's Spinetail)
- Schoutedenapus myoptilus, Teleka Kificho Scarce Swift)
- Schoutedenapus schoutedeni, Teleka wa Schouteden (Schouteden's Swift)
- Tachymarptis aequatorialis, Teleka Mabaka (Mottled Swift)
- Tachymarptis melba, Teleka Tumbo-jeupe (Alpine Swift)
- Telacanthura melanopygia Teleka-mkiasindano Mweusi (Black Spinetail)
- Telacanthura ussheri, Teleka-mkiasindano Koo-madoa (Mottled Spinetail)
- Zoonavena grandidieri, Teleka-mkiasindano wa Madagaska (Madagascar Spinetail)
- Zoonavena thomensis Teleka-mkiasindano wa Sao Tome (São Tomé Spinetail)
- Aerodramus manuoi (Mangaia Swiftlet, Holocene, Mangaia)
- Apus gaillardi (Kati hadi mwisho wa Miocene, La Grive-St.-Alban, Ufaransa
- Apus wetmorei (Mwanzi hadi mwisho wa Pliocene, Ulaya ya Kati)
- Apus baranensis (Mwisho wa Pliocene, Ulaya Kusini Mashariki)
- Apus submelba (Kati ya Pleistocene, Slovakia)
- Chaetura baconica (Mwisho wa Miocene, Hungaria)
- Collocalia buday (Mwanzo wa Miocene, Riversleigh, Australia)
- Tachornis uranoceles (Mwisho wa Pleistocene, Puerto Rico)
Teleka wa Maskarena
Teleka mdogo
Teleka wa Ulaya
Teleka mweusi
Teleka wa Bradfield
Teleka kiuno-cheupe akiruka
Teleka kiuno-cheupe ardhini
Teleka koo-kijivu
Teleka-majabali
Teleka bilachoro
Teleka-mitende
Teleka-mkiasindano wa Böhm
Teleka kificho
Teleka tumbo-jeupe