Mmenyuko wa kikemia, (pia utendanaji wa kikemia[1]; kwa Kiingereza: chemical reaction) ni mchakato ambao unasababisha mabadiliko ya dutu ya kikemia kuwa dutu tofauti.

Mfano mmojawapo ni moto (mmenyuko kati ya oksijeni hewani na kampaundi za kaboni).

Kimsingi katika mimenyuko hiyo elektroni za dutu zinazotendana zinahama na kuunda au kuondoa muungo kemia kati ya atomu husika. Mchakato ama unahitaji nishati au unaachana na nishati. Viini vya atomu havibadiliki isipokuwa kama elementi zinazoshiriki ni nururifu na nzito sana na hivyo si thabiti.

Thumb
Kama inavyoonekana kutoka mlinganyo CH </br> CH + 2 O </br> O → CO </br> CO + 2 H </br> H O, mgawo wa 2 lazima uwekwe mbele ya gesi ya oksijeni upande wa wahasibu na mbele ya maji upande wa bidhaa ili, kwa mujibu wa sheria ya utunzaji wa wingi, idadi ya kila kitu haibadiliki wakati wa athari.

Marejeo

Marejeo zaidi

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.