Lambo la Mtera ni lambo lililojengwa miaka ya 1970 kati ya mkoa wa Iringa na mkoa wa Dodoma (Tanzania) ili maji ya mto Ruaha Mkuu yaweze kutumika kuzalisha umeme (80 MW) kabla hayaendelea likielekea lambo la Kidatu.
Bwawa la Mtera ni bwawa la kufua umeme kubwa zaidi lililopo nchini (km 56 x 15).
Historia
Bwawa hili lina ukubwa wa kilomita za mraba 660 kwa uwezo kamili. Bwawa hili lina urefu wa kilometa 56 na upana wa kilometa 15 na linalishwa na mto Ruaha Mkuu na Mto Kisigo. Madhumuni ya kujengwa kwa bwawa hili ni kudhibiti kiwango cha maji katika eneo la chini la mto Ruaha lililowekwa kwa ajili ya kuzalisha umeme wa Kidatu.
Ikolojia
Bwawa hili linachukuliwa kuwa mojawapo ya maeneo bora zaidi ya kuchunguza ndege nchini Tanzania, kwa kuwa kuna takriban miti milioni moja iliyokufa ndani yake na ina maeneo mengi ya kina. Aidha, maji mengi huwa yana samaki katika bwawa hili. Mapema miaka ya 1990 takriban tani 5000 za samaki zilivuliwa bwawani.
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.