chansela mkuu From Wikipedia, the free encyclopedia
Bruno wa Wurzburg (1005 hivi - Persenbeug, Austria ya Chini, 27 Mei 1045) alikuwa chansela wa Italia (1027-1034) kwa niaba ya ndugu yake kaisari Konrad II, halafu askofu na mtawala wa Wurzburg hadi kifo chake[1][2].
Alikarabati kanisa kuu, alirekebisha maisha ya kleri na kuwafundisha waumini Maandiko Matakatifu[3].
Bruno aliandika pia kitabu cha ufafanuzi wa Zaburi na tenzi kumi za Biblia, kwa kutumia madondoo ya Mababu wa Kanisa.
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.