Moma ni spishi za nyoka wenye sumu wa jenasi Bitis katika familia Viperidae. Spishi moja huitwa bafe pia na spishi nyingine wa familia Viperidae huitwa vipiri.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Moma |
Moma wa kawaida au bafe Bitis arietans |
Uainishaji wa kisayansi |
Himaya: |
Animalia (Wanyama)
|
Faila: |
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
|
Nusufaila: |
Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
|
Ngeli: |
Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
|
Oda: |
Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
|
Nusuoda: |
Serpentes (Nyoka)
|
Oda ya chini: |
Alethinophidia (Nyoka wasio vipofu)
|
Familia: |
Viperidae (Nyoka walio na mnasaba na kipiri) Oppel, 1811 |
Jenasi: |
Bitis Gray, 1842 |
|
Ngazi za chini |
Spishi 18:
- B. albanica Hewitt, 1937
- B. arietans Merrem, 1820
- B. armata Smith, 1826
- B. atropos Linnaeus, 1758
- B. caudalis Smith, 1839
- B. cornuta Daudin, 1803
- B. gabonica A.M.C. Duméril, Bibron & A.H.A. Duméril, 1854
- B. harenna Gower, Wade, Spawls, Böhme, Buechley, Sykes & Colston, 2016
- B. heraldica Bocage, 1889
- B. inornata Smith, 1838
- B. nasicornis Shaw, 1792
- B. parviocula Böhme, 1977
- B. peringueyi Boulenger, 1888
- B. rhinoceros Schlegel, 1855
- B. rubida Branch, 1997
- B. schneideri Böttger, 1886
- B. worthingtoni Parker, 1932
- B. xeropaga Haacke, 1975
|
Funga
Spishi nyingi za moma, zile za Afrika ya Mashariki hasa, ni kubwa na nene kuliko vipiri wengine, lakini spishi kadhaa ni ndogo zaidi na moma mdogo wa Namakwa ni mdogo kabisa wa Viperidae wote duniani. Kinyume chake moma-misitu ni mkubwa kabisa.
Wakitishwa moma hutuna na kujipojaa wakifyonya kwa sauti kubwa. Inaonekana kama sio wepesi lakini wanaweza kupiga kwa kasi ya umeme.
Nyoka hawa ni wanene na wazito kwa kulinganisha na urefu wao. Wana kichwa kipana kwa umbo wa pembetatu na mkia mfupi. Magamba yao yana miinuko na yale ya pua yanaweza kuwa marefu na kufanana na pembe.
- Bitis albanica, Moma wa Albany (Albany adder)
- Bitis arietans, Bafe au Moma wa Kawaida (African puff adder)
- Bitis armata, Moma Kusi (Southern adder)
- Bitis atropos, Moma-milima Kusi (Mountain adder)
- Bitis caudalis, Moma Pembe (Horned adder)
- Bitis cornuta, Moma Pembe-nyingi (Many-horned adder)
- Bitis gabonica, Moma- au Kifutu-misitu (Gaboon viper)
- Bitis harenna, Moma wa Dodola (Dodola adder)
- Bitis heraldica, Moma wa Angola (Angolan adder)
- Bitis inornata, Moma Mfuto (Plain mountain adder)
- Bitis nasicornis, Moma-milima au Kifutu-milima (Rhinoceros viper)
- Bitis parviocula, Moma wa Bale (Bale Mountains adder)
- Bitis peringueyi, Moma Mdogo (Dwarf puff adder)
- Bitis rhinoceros, Moma Kifaru (Rhinoceros adder)
- Bitis rubida, Moma Mwekundu (Red adder)
- Bitis schneideri, Moma Mdogo wa Namakwa (Namaqua puff adder)
- Bitis worthingtoni, Moma wa Kenya au Kifutu-pembe wa Kenya (Kenya horned viper)
- Bitis xeropaga, Moma-njangwa (Desert mountain adder)
Moma-milima kusi
Moma pembe
Moma pembe-nyingi
Moma-misitu
Moma-milima
Moma wa Bale
Moma mdogo
Moma kifaru
Moma mwekundu
Moma mdogo wa Namakwa
- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
|
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Moma kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |