From Wikipedia, the free encyclopedia
Belarus (kwa Kibelarus: Беларусь (Kikyrili) au Biełaruś (Kilatini); kwa Kirusi:Белоруссия ) ni nchi ya Ulaya ya Mashariki inayopakana na Urusi, Ukraine, Poland, Lithuania na Latvia.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: -- | |||||
Wimbo wa taifa: Belarusian: Мы, беларусы (Mi Belarusi) ("Sisi Wabelarus") | |||||
Mji mkuu | Minsk | ||||
Mji mkubwa nchini | Minsk | ||||
Lugha rasmi | Kibelarus, Kirusi | ||||
Serikali Rais Waziri Mkuu |
Jamhuri Alexander Lukashenko Roman Golovchenko | ||||
Uhuru Ilitangazwa ilianzishwa ilikamilishwa |
27 Julai 1990 25 Agosti 1991 25 Desemba 1991 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
207,600 km² (ya 84) kidogo sana (183 km²)[1] | ||||
Idadi ya watu - 2016 kadirio - 2009 sensa - Msongamano wa watu |
9,498,700 (ya 93) 9,503,807 45.8/km² (ya 142) | ||||
Fedha | Rubel ya Belarus (BYN ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
FET (UTC+3) FET (UTC+3) | ||||
Intaneti TLD | .by | ||||
Kodi ya simu | +375
- |
Mji mkuu ni Minsk na miji mingine ni pamoja na Brest, Grodno, Gomel, Mogilev na Vitebsk.
Idadi ya wakazi inapungua: ni watu 9,498,700 (2016).
Belarus haikuwahi kuwa nchi ya pekee hadi karne ya 20. Maeneo yake yalikuwa chini ya himaya mbalimbali kama vile Poland, Lithuania na Urusi. Belarus ilikuwa kitengo cha Umoja wa Kisovyet tangu 1919/1922 hadi 1991.
Wakazi walio wengi ni Wabelarus (83.7%) ambao wanaongea ama Kibelarus au Kirusi ambavyo vyote viwili ni lugha rasmi. Lugha hizi mbili zina asili moja. Takriban 11% za wakazi ni Warusi.
Kuna pia vikundi vidogo vinavyotumia lugha za pekee kama vile Kipoland, Kiukraine, Kilatvia, Kilituanya na nyingine.
Walio wengi ni wafuasi wa Ukristo katika Makanisa ya Kiorthodoksi (48.3%) na katika Kanisa Katoliki (7.1%).
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.