From Wikipedia, the free encyclopedia
Bahari ya Sulu (kwa Kifilipino; Dagat ng Sulu; kwa Kiingereza: Sulu Sea) ni sehemu ya Bahari Pasifiki iliyopo kati ya Ufilipino na kaskazini mashariki mwa kisiwa cha Borneo (sehemu ya Malaysia), ikipakana upande moja na funguvisiwa la Sulu (ng'ambo yake Bahari ya Celebes) na kwa upande wa kaskazini mashariki na kisiwa cha Palawan (ng'ambo yake Bahari ya Kusini ya China). [1] [2]
Uso wa sehemu hii ya bahari ina kilomita za mraba 260,000. Kina cha wastani ni mita 1139.
Ndani ya Bahari ya Sulu iko Hifadhi ya Taifa ya Tubbataha Reef iliyoorodheshwa na UNESCO kati ya Urithi wa Dunia. [3]
Kusini magharibi mwa Bahari ya Sulu kuna visiwa ambako kasa wanatega mayai yao, hasa Kasa Uziwa (chelonia mydas) na Kasa Mwamba (eretmochelys imbricata).
Bahari ya Sulu ina historia ndefu ya uharamia uliostawi katika mapambano baina ya Wahispania (waliotawala sehemu za visiwa vya Ufilipino) na wapinzani wao wazalendo.
Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia uharamia ulipata nguvu tena. Mara nyingi ni makundi ya maharamia hadi kumi wanaoshambulia hasa maboti madogo ya mizigo na ya abiria pamoja na wavuvi. Katika miaka ya 1980 takriban mashambulio 100 yalikadiriwa kila mwaka katika Bahari ya Sulu.[4]: 60 Maharamia wa eneo hili wanahofiwa kwa sababu wanaua haraka kuliko kawaida na pia wanateka nyara.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.