Bahari ya Matumbawe
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Bahari ya Matumbawe (kwa Kiingereza: Coral Sea; kwa Kifaransa: Mer de Corail) ni sehemu ya Bahari Pasifiki mbele ya pwani ya kaskazini-mashariki ya Australia.
Inapakana na Australia, Papua Guinea Mpya, Visiwa vya Solomon na Kaledonia Mpya.
Tabianchi ni ya joto, usimbishaji ni kati ya milimita za mvua 1,000 hadi 3,000 kwa mwaka, sehemu kubwa hunyesha baina ya Desemba na Machi. Siku za Jua kuonekana ni kati ya 80 hadi 125 kwa mwaka, jotoridi hucheza kati ya sentigredi 18–27°C.
Sehemu hii ya bahari huwa imejaa visiwa vidogo na miamba tumbawe ambayo ndiyo asili ya jina lake. Mkusanyiko mkubwa zaidi wa miamba tumbawe ni Great Barrier Reef mbele ya pwani ya Australia.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.