From Wikipedia, the free encyclopedia
Awasa (pia Awassa au Hawassa, Kige'ez አዋሳ) ni mji mkuu wa Jimbo la Mataifa ya Kusini katika kusini ya Ethiopia. Iko kando la Ziwa Awasa katika Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki takriban kilomita 280 kusini ya Addis Abeba.
Mwaka 2005 Awasa ilikuwa na wakazi 125,315.[1]
Kati ya wakazi wake 69,169 wa mwaka 1994 asilimia 31,42 % walikuwa Waamhara, 24,91 % Wawelaytta, 11,55 % Waoromo, 10,2 % Wasidama, 4,85 % Wakambaata, 4,6 % Watigray, 3,23 % Soddo-Gurage, 2,15 % Wasilt'e, 2,13 % Sebat-Bet-Gurage und 1,56 % Wahadiyya.
63,42 % walisema Kiamhara kama lugha ya kwanza. [2]
Kiasili eneo la Awasa ilikuwa na misitu minene na hadi leo kuna miti mikubwa upande wa kaskazini na magharibi wa mji. Kuna maji mengi kwa hiyo watu wengi kutoka nyanda za juu walihamia hapa.
Awasa ilikuwa mji mkuu wa jimbo la awali la Sidamo. [3]
Barabara kuu kati na Addis Abeba na Nairobi inapita Awasa.
Uvuvi katika ziwa ni sehemu muhimu ya uchumi kwa wenyeji.
Kuna vyuo viwili ambavyo ni Awasa Adventist College na Chuo Kikuu cha Awasa.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.