Swala ni wanyama walao nyasi katika nusufamilia Antilopinae, Aepycerotinae na Pantholopinae za familia Bovidae. Hupatikana katika maeneo yenye nyasi fupi fupi na vichaka vifupi fupi hasa kwenye maeneo mengi ya hifadhi katika Afrika. Spishi nyingine hukimbia kilometa 80 kwa saa na zina uwezo wa kuruka mita 7 hadi 8 juu akiwa kwenye kasi. Rangi yao ni ya mchanga na nyeupe kidogo kwenye koromeo na sehemu ya chini ya mkia. Maadui yao wakubwa ni simba, chatu na chui.
- Kwa swala kama ibada ya Kiislamu, taz. Swalah.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Swala |
Swala tomi (Eudorcas thomsonii) |
Uainishaji wa kisayansi |
Himaya: |
Animalia (Wanyama)
|
Faila: |
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
|
Ngeli: |
Mamalia (Wanyana wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
|
Oda: |
Artiodactyla (Wanyama wenye vidole viwili au vinne mguuni)
|
Nusuoda: |
Ruminantia (Wanyama wanaocheua)
|
Familia: |
Bovidae (Wanyama walio na mnasaba na ng'ombe) J. E. Gray, 1821 |
|
Ngazi za chini |
Nusufamilia 3, jenasi 12:
- Aepycerotinae J. E. Gray, 1872
- Antilopinae J. E. Gray, 1821
- Ammodorcas Thomas, 1891
- Antidorcas Sundevall, 1847
- Antilope Pallas, 1766
- Dorcatragus Noack, 1894
- Eudorcas Fitzinger, 1869
- Gazella de Blainville, 1816
- Litocranius Kohl, 1886
- Nanger Lataste, 1885
- Procapra Hodgson, 1846
- Saiga J. E. Gray, 1843
- Pantholopinae Hodgson, 1834
|
Funga
- Nusufamilia Aepycerotinae
- Nusufamilia Antilopinae
- Ammodorcas clarkei, Swala Dibatag (Dibatag au Clarke's gazelle)
- Antidorcas marsupialis, Swala Mrukaji (Springbok)
- Antilope cervicapra, Swala Mweusi (Blackbuck)
- Dorcatragus megalotis, Swala Beira (Beira)
- Eudorcas albonotata, Swala wa Mongalla (Mongalla gazelle)
- Eudorcas rufifrons, Swala Paji-jekundu (Red-fronted gazelle)
- Eudorcas rufina, Swala Mwekundu (Red gazelle) – imekwisha sasa
- Eudorcas thomsonii, Swala Tomi au Swala Lala (Thomson's gazelle)
- Gazella arabica, Swala Arabu (Arabian gazelle) – imekwisha sasa
- Gazella bennettii, Swala Mhindi (Chinkara au Indian Gazelle)
- Gazella cuvieri, Swala wa Cuvier (Cuvier's Gazelle)
- Gazella dorcas, Swala-jangwa (Dorcas au Ariel Gazelle)
- Gazella erlangeri, Swala wa Neumann (Neumann's Gazelle)
- Gazella gazella, Swala-milima (Mountain Gazelle)
- Gazella leptoceros, Swala Pembe-nyembamba (Rhim Gazelle)
- Gazella saudiya, Swala wa Saudia (Saudi Gazelle) – imekwisha sasa
- Gazella spekei, Swala wa Speke (Speke's Gazelle)
- Gazella subgutturosa, Swala Mwajemi (Goitered Gazelle)
- Litocranius walleri, Swala Twiga (Gerenuk au Waller's au Giraffe-necked Gazelle)
- Nanger dama, Swala Dama (Dama Gazelle)
- Nanger granti, Swala Granti (Grant's Gazelle)
- Nanger soemmerringii, Swala wa Soemmerring (Soemmerring's Gazelle)
- Procapra gutturosa, Swala wa Mongolia (Mongolian Gazelle)
- Procapra picticaudata, Swala Goa (Goa)
- Procapra przewalskii, Swala wa Przewalski (Przewalski's Gazelle)
- Saiga tatarica, Swala Saiga (Saiga)
- Nusufamilia Pantholopinae
Swala pala
Kundi la Swala
Swala mrukaji
Swala mweusi
Swala paji-jekundu
Swala mhindi
Swala wa Cuvier
Swala-jangwa
Swala-milima
Swala wa Sahara
Swala mwajemi
Swala twiga
Swala dama
Swala granti
Swala wa Soemmerring
Swala Goa
Saiga
Pembe za Swala
Swala na Nyumbu
Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.
|
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Swala kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |