From Wikipedia, the free encyclopedia
Alfa (Α au α) na omega (Ω or ω) ndizo herufi ya kwanza na ya mwisho ya alfabeti ya Kigiriki.
Kwa sababu hiyo zimechukuliwa kama ishara ya mwanzo na mwisho.
Kitabu cha Ufunuo (1:8, 21:6 na 22:13)[1] kinazitumia pamoja kama jina la Yesu Kristo na la Mungu[2][3], kwa kuwa ndio asili na kikomo cha viumbe vyote.
Maandishi ya Uyahudi yanasema kuwa neno emet (אמת, yaani "uaminifu"), moja ya sifa kuu za YHWH, linaundwa na herufi ya kwanza, ya kati na ya mwisho wa alfabeti ya Kiebrania.
Qur'an (57:3) inataja al'Awwal (الأول), yaani "Wa Kwanza" na al'Akhir (الآخر), yaani "Wa Mwisho" kati ya majina ya Allah.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.