From Wikipedia, the free encyclopedia
Aleksanda I wa Aleksandria (alifariki tarehe 26 Februari[1] au 17 Aprili, 326 au 328) alikuwa Patriarki wa 19 wa Aleksandria, Misri, maarufu kwa imani na juhudi.
Wakati wa uongozi wake alikabili masuala mbalimbali, kama vile tarehe ya Pasaka, matendo ya Meletius wa Lycopolis, na hasa Uario. Ndiye aliyekuwa mpinzani mkuu wa padri Ario na wa mafundisho yake hadi Mtaguso wa kwanza wa Nisea, ambao aliushiriki uzeeni pamoja na maaskofu wengine 317 na ambao ulikataa uzushi huo hata kwa kutunga kanuni ya imani sahihi. Ndiye aliyemuandaa shemasi Atanasi wa Aleksandria kuwa mwandamizi wake.[2]
Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki, Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu[3].
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Februari[4] au 29 Mei[5].
Mengi kati ya maandishi yake hayakutufikia, isipokuwa barua mbili. Mengine hayana hakika.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.