Alberto wa Sarteano

From Wikipedia, the free encyclopedia

Alberto wa Sarteano (Sarteano, 1385 - Milano, 15 Agosti 1450[1]) alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo na kasisi wa Kanisa Katoliki.

Alijiunga na urekebisho wa Waoservanti mwaka 1415 akashirikiana hasa na Bernardino wa Siena akawa makamu wa mkuu wa shirika lote [2]. Pamoja na Yohane wa Kapestrano na Yakobo wa Marka, hao wawili ndio wanaohesabiwa nguzo ya tawi hilo.

Kutokana na sifa yake kubwa, anaheshimiwa kama mwenye heri.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 15 Agosti.

Tazama pia

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.