Airkenya

From Wikipedia, the free encyclopedia

Airkenya

Airkenya Express ni aina ya ndege iliyo na makao mjini Nairobi, Kenya. Airkenya husafirisha watu kote nchini Kenya na hata pia hadi Tanzania. Makao yake makuu ni katika Uwanja wa ndege wa Wilson, Nairobi.[1]

Thumb
Ndege ya Airkenya aina ya Dash 7

Historia

Thumb
Picha rasmi ya Airkenya mnamo mwaka 1990

Airkenya Express ilianza kazi mwaka 1987 kutoka kwa kuunganishwa kwa Air Kenya na Sunbird Aviation. Makampuni haya mawili yalikuwa na uzoefu katika anga wa zaidi ya miaka 20 katika Afrika Mashariki. Airkenya Aviation ilibadilishwa kuwa Airkenya Express mnamo Januari 2007. Kampuni hii inamilikiwa na wanabiashara Wakenya na ina wafanyakazi 165.[1]

Huduma

Airkenya inatoa huduma zifuatazo (mnamo Septemba 2007) [2]:

Safari za nchini Kenya:

  • Amboseli (Uwanja wa ndege wa Amboseli)
  • Lamu (Uwanja wa Ndege wa Manda)
  • Lewa Downs (Uwanja wa ndege wa Lewa)
  • Malindi (Uwanja wa Ndege wa Malindi)
  • Maasai Mara (Uwanja wa ndege wa Mara Serena)
  • Meru (Uwanja wa ndege wa Mulika Lodge)
  • Mombasa (Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Moi)
  • Nairobi (Uwanja wa ndege wa Wilson)
  • Nanyuki (Uwanja wa ndege wa Nanyuki)
  • Samburu (Uwanja wa Ndege wa Samburu)

Safari za Kimataifa:

  • Kilimanjaro (Uwanja Wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro

Ndege

Airkenya inajumuisha ndege zifuatazo (mnamo Machi 2007):[1]

  • 1 Bombardier Dash 8
  • 2 Bombardier Dash 7 Series 100
  • 3 De Havilland Kanada DHC-6 Twin Otter Series 300

Viungo vya nje

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.