![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/9/94/ShrinkingLakeChad-1973-1997-EO.jpg/640px-ShrinkingLakeChad-1973-1997-EO.jpg&w=640&q=50)
Chad (ziwa)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ziwa Chad ni ziwa kubwa lisilo na njia ya kutoka lenye kina kidogo katika kanda la Sahel, kando ya jangwa kubwa la Sahara, kule ambako nchi za Chad, Kamerun, Niger na Nigeria zinapopakana, hivi kwamba eneo lake limegawanywa kati ya nchi hizo. Ziwa Chad lina umuhimu mkubwa kwa uchumi wa watu milioni 68 katika nchi hizo nne.
Ukweli wa haraka Ziwa Chad ...
| |
Mahali | Afrika ya Kati |
Nchi zinazopakana | Chad, Kamerun, Nigeria, Niger |
Eneo la maji | 1500 km² |
Kina cha chini | hadi 7 m |
Mito inayoingia | Chari, Komadugu, Logone |
Mito inayotoka | --- |
Kimo cha uso wa maji juu ya UB |
m 240 |
Miji mikubwa ufukoni | -- |
Funga
Beseni lake ni beseni kubwa le bara la Afrika. Hata hivyo, eneo la uso wake limebadilika katika mwendo wa karne zilizopita kutegemeana na kiasi cha maji lilichopokea na kiwango cha uvukizaji na matumizi ya maji yake.
Ziwa Chad lilipungua kwa asilimia 98 baina ya miaka 1963 na 1998 lakini picha za satelaiti za ESA zimeonyesha ya kwamba baada ya hapo limepanuka tena kiasi. [1]