From Wikipedia, the free encyclopedia
Zinki ni elementi yenye namba atomia 30 kwenye mfumo radidia, uzani atomia ni 65.409. Alama yake ni Zi.
Zinki (zincum) | |
---|---|
Zinki | |
Jina la Elementi | Zinki (zincum) |
Alama | Zn |
Namba atomia | 30 |
Mfululizo safu | Metali ya mpito |
Uzani atomia | 65.409 |
Valensi | 2, 8, 18, 2 |
Densiti | 7.14 g/cm³ |
Ugumu (Mohs) | 2.5 |
Kiwango cha kuyeyuka | 692.68 K (419.53°C) |
Kiwango cha kuchemka | 1180 K (907 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 0.01 % |
Hali maada | mango |
Katika mazingira ya kawaida ni metali yenye rangi ya buluu-nyeupe. Kiwango chake cha kuyeyuka ni 1,180 C°.
Hupatikana ndani ya madini, haitokei kiasili kama elementi tupu. Huchimbwa hasa China, Peru, Australia, Kanada, Marekani, Meksiko na Afrika Kusini.
Matumizi ya zinki ni takriban tani milioni 11 (kwa mwaka 2006). Takriban nusu yake ni kwa kuzuia ubabuzi (kutokea kwa kutu) wa mabati au vifaa vingine vya chuma kwa njia ya galvania n.k..
Vinginevyo hutumiwa katika aloi kama shaba nyeupe na hasa kutengeza betri.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Zinki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.