Yohane wa Shanghai na San Francisco
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yohane wa Shanghai na San Francisco (kwa Kirusi: Иоанн Шанхайский и Сан Францисский, Ioann Shankhayskiyi i San Frantsiskyi; jina la awali: Михаил Борисович Максимович, Mikhail Borisovich Maximovitch; Adamovka, wilaya ya Izyum, mkoa wa Kharkov, leo nchini Ukraina, 4 Juni 1896 – Seattle, Washington, USA, 2 Julai 1966) alikuwa mmonaki, padri, askofu na mmisionari wa Kiorthodoksi huko China na Marekani.
Alijulikana pia kwa karama ya kutenda miujiza.
Alitangazwa na Kanisa lake kuwa mtakatifu tarehe 2 Julai 1994.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe hiyohiyo.