Yohakimu wa Fiore
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yohakimu wa Fiore, O.Cist., au wa Flora (kwa Kiitalia Gioacchino da Fiore) alikuwa mmonaki wa Italia kusini (Celico, leo mkoani Calabria, 1135 hivi – San Martino di Canale, Calabria, 30 Machi 1202) aliyeanzisha abasia ya San Giovanni in Fiore na shirika lilitokana na lile la Citeaux.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/e/ec/Joachim_of_Flora.jpg)
Ni maarufu kwa mafundisho yake ambayo baadaye yalikuja kulaaniwa na Kanisa Katoliki kama ya kizushi.
Hata hivyo mwenyewe hakuwa na nia hiyo, bali alimwekea Papa maamuzi yoyote juu yake. [1]
Kwa sababu hiyo shirika lake, likizingatia uadilifu wake wa kishujaa, liliwahi kumtangaza mwenye heri, na sasa jimbo lake la Cosenza-Bisignano linaendelea na kesi ya kumtambua hata mtakatifu.