Yamuna
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yamuna (kwa Kihindi: यमुना, yamunā; pia: जमुना, Jamuna; kwa Kiurdu: جمنا) ni mto mkubwa huko Uhindi Kaskazini. Ni tawimto kubwa zaidi la mto Ganga.
Ukweli wa haraka Mto Yamuna ...
Chanzo | milima ya Himalaya katika jimbo la Uttarakhand |
Mdomo | mto Ganga |
Nchi | Uhindi |
Urefu | km 1,376 |
Kimo cha chanzo | mita 3,293 |
Tawimito upande wa kulia | mito ya Chambal, Betwa, Ken, Sindh, Baghain |
Tawimito upande wa kushoto | miro ya Hindon, Tons, Giri, Rishiganga, Hanuman Ganga, Sasur Khaderi |
Mkondo | wastani m3 2,950 |
Eneo la beseni | km2 366,223 |
Miji mikubwa kando lake | Delhi, Mathura, Agra, Allahabad |
Funga
Huanza kwenye milima ya Himalaya katika jimbo la Uttarakhand. Unaendelea katika majimbo ya Uhindi ya Haryana, eneo la mji mkuu Delhi na Uttar Pradesh. Mwishowe, kwenye mji wa Allahabad, inaishia katika mto Ganga baada ya mwendo wa kilomita 1,370.
Matawimto yake muhimu zaidi ni mito Tons na Chambai.