![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/c/c6/10th_all_china_games_floor.jpg/640px-10th_all_china_games_floor.jpg&w=640&q=50)
Wushu - (Kung Fu)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Wushu (/ˌwuːˈʃuː/), au Kungfu ya Kichina, ni mchezo wa upiganaji ulioanzishwa nchini China.[1][2] Jina "Wushu" linatokana na maneno ya Kichina (武 "Wu" = kijeshi, kwa Kiingereza military or martial, na 術 "Shu" = Sanaa, kwa Kiingereza arts).
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/c/c6/10th_all_china_games_floor.jpg/640px-10th_all_china_games_floor.jpg)
Wushu umekuwa mchezo wa kimataifa kupitia Shiririkisho la Kimataifa la Wushu (IWUF - International Wushu Federation). Shirikisho hili ndilo huendeleza michezo ya kimataifa ya wushu kama vile Michuano ya Dunia ya Wushu inayofanyika kila baada ya miaka miwili tangu shindano la kwanza mwaka wa 1991 Beijing, China.