Upofu wa mto(ni) au usubi (pia inajulikana kama Onchocerciasis na Maradhi ya Robles), ni maradhi yasababishwayo na ambukizo la kinyoo wa kimelea Onchocerca volvulus.[1]
Dalili ni pamoja na mwasho mkali, manundu chini ya ngozi, na upofu. Maradhi hayo ni sababu ya pili baada ya vikope kumfanya mtu kuwa kipofu kutokana na ambukizo.[2]
Chanzo na uaguaji
Mwaka wa 1915 daktari Rodolfo Robles aligundua kwa mara ya kwanza uhusiano baina ya kinyoo na maradhi ya macho.[3]
Kinyoo cha kimelea anasambazwa na maumo ya usubi weusi wa spishi fulani za jenasi Simulium.[1] Kwa kawaida maumo mengi yanahitajika kabla ya ambukizo kuumiza.[4]
Usubi hao huishi karibu na mito: ndiyo sababu ya jina “upofu wa mto”.[2]
Mara tu vinyoo wameshaingia mwilini wanaunda kiluwiluwi ambao wanatembea hadi nje, juu ya ngozi ambapo wanaweza kumwambukiza nzi aliyekuja kuuma binadamu husika.[1]
Utambuzi
Kuna namna kadhaa za kufanyia uanguaji nazo ni pamoja na: kutia tishu ya ngozi iliyokatwa ndani ya mchanganyiko wa maji yenye asilimia 0.9 ya chumvi ukasubiri kiluwiluwi kutokea, kuchunguza jicho kwa dalili za kiluwiluwi, na kuchunguza manundu yaliyo chini ya ngozi kugundua vinyoo wazima.
Kinga na tiba
Hakuna dawa ya chanjo dhidi ya maradhi hayo. [1] Ugangakinga ni kujiepusha na kuumwa na nzi.[5]
Namna za kusaidia kujiepusha ni pamoja na dawa za kinga dhidi ya vidudu na mavazi yanayofaa. [5] Taratibu zingine ni zile za kupunguza idadi ya nzi kwa kupulizia dawa za kuua wadudu.[1]
Bidii zenye kufutilia kabisa maradhi hayo katika dunia nzima kwa kuwatibu mara mbili kwa mwaka watu walio pamoja katika makundi zinatendeka sehemu kadhaa za dunia.[1]
Matibabu ya wale walioambukizwa ni kuwapa dawa ya ivermectin kila baada ya miezi sita au miezi kumi na mbili.[1][6] Matibabu hayo huua kiluwiluwi lakini hayawaui vinyoo wazima.[7]
Dawa ile ya doxycycline ambayo huua bakteria waitwao Wolbachia nayo ikihusika na [[endosymbiont] inaonekana kudhoofisha vinyoo ikapendekezwa vilevile.[7] Upasuaji wenye kuondoa manundu vilevile unatendeka. [6]
Takwimu
Takriban watu milioni 17 hadi 25 wanaambukizwa upofu wa mto, huku takriban milioni 0.8 wamekosa kiasi fulani cha uwezo wa kuona.[4][7]
Maambukizo kwa wingi hutokea barani Afrika kusini kwa Sahara, ingawa wengine wanaoishi Yemen pamoja na sehemu za upweke za Amerika ya Kati na Amerika ya Kusini wameambukizwa.[1]
Maradhi hayo yanaelezwa kuwa maradhi ya nchi za joto yasiyoangaliwa na Shirika la Afya Duniani. [8]
Marejeo
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.