Ugonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofungana
faida ya kitunguu saumu / From Wikipedia, the free encyclopedia
Ugonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofungana (unaojulikana pia kama Ugonjwa sugu wa mapafu yaliyofungana, ugonjwa sugu wa mapafu yaliyofungana, ugonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofungana na ugonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofunana pamoja na majina mengine), ni aina ya ugonjwa wa mapafu yaliyofungana unaodhihirika kwa hali duni na sugu ya upitaji wa pumzi. Hali hii kwa kawaida huendelea kuwa mbaya zaidi baada ya muda. Dalili zake kuu ni kupungukiwa na pumzi, kukohoa, na kutoa makohozi.[1] Watu wengi walio na bronkitisi sugu wana ugonjwa sugu wa mapafu yaliyofungana.[2]
Chronic Obstructive Pulmonary Disease | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Specialty | Pulmonology |
ICD-10 | J40.–J44., J47. |
ICD-9 | 490–492, 494–496 |
OMIM | 606963 |
MedlinePlus | 000091 |
eMedicine | med/373 emerg/99 |
MeSH | C08.381.495.389 |
Uvutaji tumbaku ndio kisababishi kikuu cha ugonjwa sugu wa mapafu yaliyofungana, pamoja na vipengele vingine kama vile uchafuzi wa hewa huku jenetikia ikichangia kwa kiwango kidogo.[3]
Katika nchi zinazoendelea, chanzo kikuu cha uchafuzi wa hewa ni kupikia au kuwasha moto mahali pasipo hewa ya kutosha. Mazingira ya muda mrefu wa miwasho hii husababisha mwitikio wa inflamesheni kwenye mapafu, hivyo kupelekea njia za pumzi kuwa nyembamba na kuharibika kwa tishu za mapafu, hali iitwayo emfisema.[4]
Utambuzi huo ni kwa msingi wa hali duni ya kupita kwa pumzi kama ilivyopimwa kwa kipimo cha utendakazi wa mapafu.[5]
Ugonjwa sugu wa mapafu yaliyofungana unaweza kuzuiliwa kwa kupunguza uhatarisho wa visababishi vinavyojulikana. Hii hujumuisha juhudi za kupunguza viwango vya uvutaji na kuboresha hali ya hewa ya ndani na nje ya majengo. Mbinu za matibabu ya ugonjwa huu ni kuacha uvutaji, chanjo, urekebeshaji mapafu, na mara nyingi vipanua bronkasi vya kupumuliwa na steroidi.
Kinyume na pumu, hali ya upitaji wa pumzi haiboreshwi sana na matibabu. Baadhi ya watu wanaweza kunufaika na matibabu ya oksijeni ya muda mrefu au kupandikiza mapafu.[4] Kwa watu walio na vipindi vya kuzidi kwa ugonjwa sugu wa mapafu yaliyofungana, ongezeko la utumiaji dawa na kulazwa hospitalini kunaweza kuhitajika.
Duniani kote, ugonjwa sugu wa mapafu yaliyofungana huathiri watu milioni 329 au takriban asilimia 5 ya idadi yote ya watu. Mwaka 2011, ugonjwa huo ulikadiriwa kuwa kisababishi kikuu cha nne cha vifo, ukiwaua zaidi ya watu milioni 3 .[6] Idadi ya vifo imetabiriwa kuongezeka kutokana na viwango vya juu vya uvutaji na idadi ya watu wanaozeeka katika nchi nyingi.[7]
Ugonjwa huu ulisababisha hasara ya kiuchumi iliyokadiriwa kuwa dola trilioni 2.1 mwaka 2010.[8]