Tuzo ya Pulitzer ya Bunilizi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Tuzo ya Pulitzer ya Bunilizi ni aina moja ya Tuzo za Pulitzer ambazo hutolewa kila mwaka nchini Marekani. Ni miongoni mwa aina za asili zilizotolewa kuanzia 1917 ambapo iliitwa Tuzo ya Pulitzer ya Riwaya (hadi 1947). Tuzo ya Bunilizi humheshimu mwandishi Mwarekani aliyetoa andiko la bunilizi katika mwaka uliopita.
Kuanzia 1980, wagombea watatu wa mwisho walikuwa hutangazwa, yaani mshindi mkuu pamoja na mshindi wa pili na wa tatu.