Trakoma
From Wikipedia, the free encyclopedia
Trakoma (inaitwa pia: vikope, Egyptian ophthalmia[1]) ni ugonjwa wa maambukizi unaosababishwa na bakteria Klamidia trakomati.[2] Maambukizi husababisha kukwaruza kwa sehemu ya ndani ya vigubiko vya macho. Huo mkwaruzo unaweza kusababisha maumivu ya macho, kuharibika kwa sehemu ya nje ya macho au konea, na hatimaye upofu.[2]