Tekla wa Ikonio
From Wikipedia, the free encyclopedia
Tekla wa Ikonio (kwa Kigiriki: Θέκλα, Thékla) alikuwa mwanamke wa mji huo wa Likaonia (leo nchini Uturuki) katika karne ya 1 BK.
Inasemekana alipata kuwa mfuasi wa Mtume Paulo, inavyosimuliwa na kitabu cha karne ya 2 Matendo ya Paulo na Tekla (180 hivi).
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki na Waanglikana kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe tofautitofauti: 23 Septemba, 24 Septemba au 3 Oktoba.